DC MPOGOLO : SINA TAARIFA UWEPO WA KIFUSI CHENYE KEMIKALI KATA YA MZINGA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, September 24, 2024

DC MPOGOLO : SINA TAARIFA UWEPO WA KIFUSI CHENYE KEMIKALI KATA YA MZINGA

 


NA MAGENDELA HAMISI


WAKATI Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mzinga, Kata ya Mzinga wilayani Ilala, Daniel Nyaiko, akibainisha kwamba Mkuu wa Wilaya hiyo, Edward Mpogolo, tayari amepeleka wataalamu kupima udongo unaolalamikiwa na wananchi wakidhani unaweza kuwa kemikali, Mkuu huyo wa Wilaya amekanusha na taarifa hiyo.


"Wewe ndio unanipa taarifa hizo, mimi sijui kwangu hazijafika, inawezekana hiki ni kipindi cha uchaguzi, pengine wananchi hao hawamtaki Mwenyekiti, sasa waambie wakajiandikishe kupiga Kura,


"Kwa sababu ulitakiwa kuwauliza hicho kifusi, kimetoka wapi au katika kiwanda gani hapo ndipo tuanze uchunguzi," amesema.


Wakati Mpogolo akikanusha kuwa na taarifa hiyo, awali mwenyekiti wa mtaa huo, Nyaiko, alimweleza mwandishi wa habari  hizi kwamba kufuatia wasiwasi uliotanda kwa wananchi kuhusu kifusi kilichomwagwa barabani wakidai kuwa na kemikali kutokana na athari zinazojitokeza, tayari jopo la wataalamu nane kutoka kwa mkuu wa wilaya hiyo walifika jana, Septemba 24, 2024 na wamechukua sampuli ya udogo unaolalamikiwa kwa ajili ya kupima  na Ijumaa Septemba 27, 2024 majibu yatarejeshwa na wananchi wataelezwa.


Malalamiko ya wananchi kuhusu kifusi hicho ambacho kimemwagwa katika barabara ya Nyangasa eneo la Kwanyoso yalianza tangu, 2021 baada ya athari ya bati za nyumba zao kuanza kupata kutu na kutoboka kabla ya muda sahihi.


Alifafanua zaidi mkazi wa eneo hilo, Matokeo Charles, amesema " baada ya kifusi hicho kumwagwa, mvua ziliponyesha tu maji yaliyotiririka kutoka kwenye bati yalionesha kuwa chembeche zenye mn'gao.


"Hali hiyo ikafuatiwa na mabati kupata kutu na kutoboka kabla ya wakati kwa kuwa zilikuwa mpya na zisingeweza kupata kutu kwa haraka na kutoboka, pia wakati kifusi hicho kinamwagwa kilikuwa na vipande vingi vya chuma ambavyo viliokotwa kama chakavu na kuuzwa" ameongeza.


Pia alisema kwamba baada ya kadhia hiyo kujitokeza walifiksha taarifa kwa mwenyekiti wa mtaa huo, ambaye inadaiwa ndiye aliyekimwaga eneo hilo kwa ajili ya kufukia mashimo yaliyokuwa kwenye barabara hiyo.


Ameongeza licha ya kufikisha malalamiko hayo wakadai hayakufanyiwa kaz,  badala yake waliambiwa kuwa ni wapinzani wa kisiasa na wapinga Maendeleo.


Kutokana na kutosikiliza waliamua kuyafikisha malalamiko yao kwa njia ya barua kwa diwani wao, Mtendaji Kata, Mkurugenzi wa Jiji la Ilala, Kwa Mkuu wa wilaya hiyo wa wakati huo,  Mwilabuzi Ludigija, pamoja na  Baraza la Taifa la Mazingira( NEMC).


Matokeo, anadai baada ya hatua hizo, NEMC walipeleka  wataalamu wao na kuchukua sampuli ya mchanga na hadi sasa hakuna majibu yaliyorejeshwa kweo ili hali athari zinazidi kuongezeka" amesema.


 Pia anafafanua kwamba wakati changamoto hiyo inajitokeza kulikuwa na nyumba zipatazo 19 ambazo ziliathirikia na anadai zinakaribia 40 ambazo mabati yametoboka nakusababisha hasara kubwa kwa wananchi hao.



Naye Mjumbe wa Kamati katika Msikiti wa Nurhuda ambao upo pembezoni mwa barabara hiyo, Ustadhi Juma Ally ,amesema baada ya hadha hiyo kutokea, tayari wamebadilisha bati ingawa nazo kwa muda mfupi zimeanza kupata kutu na kutoboka. 


"Tunaomba, Rais atusaidie,watendaji wake huku chini wanaonekana wameshindwa kutusaidia,sisi ni wananchi wake, hatuna pesa kubadilisha bati kila mara,tumetoa malalamiko yetu kwa muda mrefu lakani hatusaidii na hawa wasaidizi wake  "amesema.



Pia, Ombi Sanga mkazi wa mtaa huo, amesema kuwa inashangaza wanapotoa malalamiko yao kwa viongozi wao wanasemwa kwamba wao ni wapinga maendeleo na kwamba wanatumiwa kisiasa jambo ambalo amedai sio la kweli, wanachotaka wao ni kifusi hicho kiondokewe na kiwekwe kingine.


"Sijui ninj kinawashinda wakati athari zinazidi, tunamuomba Rais atusikilize ili atusaidie kutuondokea kero kwani wasaidizi wake wameshindwa.


"Kwakweli hali hii inatuumiza mno kwa muda mrefu sasa, tunaomba Mama( Rais Samia) atusaidie, kwa maana viongozi wa huku chini wameshindwa kabisa kutusaidia,tunateseka na changamoto hii" amesema



No comments:

Post a Comment