KAPINGA AFUNGUA KIKAO KAZI TPDC - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, September 17, 2024

KAPINGA AFUNGUA KIKAO KAZI TPDC


*Awataka kuyapa kipaumbele masuala ya wafanyakazi.


NA MWANDISHI WETU

NAIBU Waziri Nishati, Judith Kapinga leo Septemba 17, 2024 amefungua kikao kazi cha Menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Jijini Mwanza.


Lengo la kikao hicho ni kujitathmini, kujipanga na kukumbushana masuala mbalimbali ya Taasisi, ikiwemo maelekezo mbalimbali ya Serikali ya uendeshaji wa kampuni.


Pia amewasisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa umoja, ubunifu, weledi na upendo baina ya uongozi wa TPDC na  wafanyakazi.


" Wizara ipo pamoja nanyi kuhakikisha azma na malengo makuu ya Serikali kwa TPDC yanafikiwa na zaidi", amesisitiza Kapinga. 


Aidha, amewakumbusha kuendelea kuyapa mkazo masuala yanayohusu wafanyakazi kwani ndio  kiungo muhimu cha kufanikiwa kwa mipango na malengo mbalimbali ya TPDC.


"Ni vema masuala yanayohusu motisha zao ikiwemo mishahara kuhuishwa inapobidi na kuboreshwa kama hali ya kifedha inaruhusu", Amesema Mhe. Kapinga.


Ameongeza kuwa itasaidia kuwapa morali ya kuendelea kufanya kazi TPDC na kuvutia pia wafanyakazi wazuri sokoni.


Ametaka changamoto za wafanyakazi kukaimu nafasi za uongozi muda mrefu bila kuthibitishwa na changamoto za kupandishwa madaraja na nyinginezo zifanyiwe kazi ili kupunguza malalamiko kwa wafanyakazi.






No comments:

Post a Comment