MHASIBU WILAYA YA MTAMA KIZIMBANI KWA MAKOSA YA RUSHWA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, September 3, 2024

MHASIBU WILAYA YA MTAMA KIZIMBANI KWA MAKOSA YA RUSHWA


SEPTEMBA 3, 2024 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi, imefunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi Namba  25141/2024 Jamhuri dhidi ya BAKARI ISSA NGUMBA - Mhasibu Msaidizi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama.


Mshitakiwa anakabiliwa na makosa mawili ambayo ni kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri Kinyume na Kifungu cha 22 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 32 Marejeo ya Mwaka 2022 kikisomwa pamoja na   Aya ya 21 ya Jedwali la kwanza pamoja na kifungu cha 57(1) na  60(2) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 Marejeo ya mwaka 2022. 


Kosa lingine ni Kughushi kinyume na Kifungu cha 333,335(a) na 337 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 Marejeo ya Mwaka 2022.


Mshitakiwa akiwa  Mhasibu Msaidizi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama, kati ya tarehe 31 Desemba 2021 na 31 Januari 2022, alighushi  Orodha ya malipo pamoja na Hati ya malipo inayoonesha kuwa alimlipa dereva wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama kiasi cha shilingi laki sita na elfu hamsini tu(650,000/=) kama malipo kwa ajili ya kazi ya usimamizi  wa miradi ya maendeleo vijijini jambo ambalo halikuwa kweli.


Aidha mshtakiwa aliwasilisha nyaraka  hizo zilizoghushiwa kwa mwajiri wake ili aidhinishe malipo hayo.


Baada ya kusomewa hati ya mashtaka mshtakiwa alikana makosa yote mawili na akakamilisha masharti ya dhamana.


Kesi  imepangwa kuja kwa kusomwa hoja za awali tarehe 2/10/2024.


Kesi hii inaendeshwa na  wakili wa serikali Salum Bhoki wa TAKUKURU Lindi.

No comments:

Post a Comment