NA DOTTO MWAIBALE
MJUMBE wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Dkt. Zakia Abubakar amewataka Maofisa Uandikishaji Ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa Teknolojia ya Habari (TEHAMA) wa Halmashauri kuzingatia maelekezo yote yatakayo tolewa na Tume ili waweza kufanya kazi kwa wakati pindi zoezi la uandikishaji wapiga kura kwenye Daftari la Kudumu litakapoanza.
Dkt. Abubakar ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo kwa watendaji hao ngazi ya mkoa kuhusu uboreshaji wa Daftrai la Kudumu la Wapiga Kura kwa maafisa waliotajwa hapo juu mafunzo yaliyoanza Septemba 14, 2024 katika Ukumbi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida.
“Matokeo bora ya zoezi hili yatategemea uwepo wa ushirikiano mkubwa kati ya watendaji wote wa uboreshaji Serikali, Vyama vya Siasa na Wadau wengine wa uchaguzi,” alisema Abubakar.
Abubakar aliwasihi maofisa hao kuwa na ushirikiano wa karibu na Tume wakati wote ambao watakuwa wakitekeleza majukumu yao na watakapokuwa na jambo ambalo watahitaji ufafanuzi au changamoto yoyote wasisite kuwasiliana na Tume,” alisema Abubakar.
Mafunzo hayo yanawajengea umahiri wa kuwafundisha Maofisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata ambapo nao watatoa mafunzo hayo kwa Waendeshaji wa Vifaa vya Bayometriki na Waandishi Wasaidizi ambao ndio watahusika na uandikishaji wa wapiga kura vituoni.
Aidha, Maofisa TEHAMA watapatiwa mafunzo maalum ya jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiufundi endapo zitajitokeza wakati wa zoezi la uandikishaji wa wapiga kura vituoni.
“ Nimejulishwa kuwa, baadhi yenu mlibahatika kushiriki katika kuratibu na kusimamia utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Tume ikiwemo uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga kura katika awamu zilizopita kwa kutumia uzoefu mlionao na mafunzo mtakayopatiwa, ninaamini mtafanya kazi zenu kwa weledi, bidii na moyo wa kujituma ili kufanikisha zoezi hili,” alisema Dkt. Abubakar.
Dkt. Abubakar aliwasihi kutumia uzoefu walionao kuwasaidia wenzao ambao hawakuwahi kushiriki katika zoezi kama hili ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu.Vilevile, wakati wa uboreshaji wa Daftari mawakala wa
No comments:
Post a Comment