WATOTO WA MAUNDA ZORRO WAMLIZA MONALISA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, September 7, 2024

WATOTO WA MAUNDA ZORRO WAMLIZA MONALISA

 


NA MWANDISHI WETU

WAKATI akitambulisha baadhi watu ambao wamefika katika shughuli ya kuwakumbuka na kuwasomea dua wasanii, ambao wametangulia mbele ya haki, Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya shughuli hiyo, Yvonne Cherrie 'Monalisa' amemwaga chozi baada ya kutaja majina ya watoto wa msanii, Maunda Zorro.


 Shughuli ya kuwaombea dua wasanii zaidi ya 250 ambao wametangulia mbele ya kwa miaka tofauti imefanyika jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Leader.

 

"Nawaona watoto wa rafiki, ndugu yangu, Maunda Zorro ..... Choziii.... , Mungu awabariki sana na jambo hili la kuwaombea wasanii, litaendelea na huu ni mwanzo,  hadi sasa idadi ya wasanii wenzetu ambao wametangulia mbele ya haki ni zaidi ya 250 na tutaendelea kuondoka na hatujui nani baada ya hapa ataanza, amesema. 


No comments:

Post a Comment