MKULIMA KIJIJI CHA GEDAMAR WILAYANI BABATI ATOA SOMO KILIMO CHA JAMII YA MIKUNDE - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, October 20, 2024

MKULIMA KIJIJI CHA GEDAMAR WILAYANI BABATI ATOA SOMO KILIMO CHA JAMII YA MIKUNDE

 

    Zao jamii ya mikunde ikiwa shambani. (Picha kwa hisani ya Mtandao)


NA MIKE MANDE

DODOO Matambo, mkulima mdogo kutoka kijiji cha Gedamar katika kata  ya Galapo, wilayani Babati amesema kuwa ni vyema kwa wakulima wadogo kulima zao la jamii ya mikunde kwa njia ya umwagiliaji ili kujipatia kipato na kuweza kuweza kuukabili ukame.

 

Matambo amesema kuwa kilimo cha umwagiliaji ndiyo suluhisho pekee la kumkomboa mkulima mdogo ili aweze kulima wakati wote katika mazao ambayo kwa sasa yameanza kuuzwa kwa bei ya juu.

 

Mkulima huyo ambaye anamiliki shamba la heka moja na nusu na kumwagilia kwa njia yam atone, amesema kuwa aliamua kujiingiza katika kilimo hicho baada ya ukame ulioukumba kijiji hicho mwaka 2022.

 

“Niliona ni vyema kuanza kuchimba kisima na kulima kilimo cha umwagilaiji. Baadaye nilipata mafunzo kutoka Beula Seed Co & Sons Ltd na kupata mbegu bora na sasa naona faida yake,” alisema Matambo.

 

Mradi huo ambao unafadhali na Taasisi ya Kukuza na Kuendeleza Mifumo ya Masoko nchini (AMDT) una lengo la kuwasadia wakulima wadogo kuacha kutegemea mvua za vuli na badala yake kutumia kilimo cha umwagiliaji kwa kuchimba visima na kutoka vianzo vya karibu vya maji.

 

Delta Shila, Delta Shila, Mratibu wa Tathmini na Ufuatiliaji wa Matokeo wa AMDT anasema kuwa mradi huo pia una lengo la kuinua kilimo cha jamii ya mikunde ikiwemo maharagwe, mbaazi, kunde na choroko ili kiweze kutumika  kwa wingi nchini.

 

“Tunataka wakulima waliyo katika mradi wetu kuzidi kufaidika na kupanda kwa bei na kujipatia virutubisho vilivyo katika mazao hayo kwa familia zao na pia kuwafanya wakulima hao kusaidia kuzalisha mbegu bora,” alisema Shila.

 

Kwa mujibu wa Shila, mradi wa umwagiliaji unaondeshwa na AMDT katika maeneo mbali mbali nchi umewezesha wakulima wengi kujifunza jinsi wenzao wanavyo wafanikiwa.

 

No comments:

Post a Comment