NA MAGENDELA HAMISI
WAKALA
wa Usajili wa Biashaa na Leseni (BRELA), Oktoba 25 mwaka huu, wanatarajia
kukutana na wadau wake kutoka sekta ya umma na sekta binafsi kwa lengo la
kujadili fursa, mafanikio na changamoto za biashara kwa ujumla.
Katika taarifa iliyotolewa leo Oktoba 23,
mwaka huu na Kitengo cha Mawasiliano cha BRELA, imesema kwamba mkutano huo ni
wapi pili kufanyika utawakutanisha washiriki wapatao 300 kutoka taasisi
mbalimbali nchini na dhumuni likiwa ni kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi
hiyo na wadau wake.
Pia
imesema kwamba dhumuni lingine ni kuwajengea uelewa wa pamoja kuhusu huduma
zinazotolewa na BRELA na taasizi zingine zinazoratibu urasimishaji wa biashara
nchini huku Kauli mbiu ya mkutano huo ni , “Mifumo ya Kitaasisi inayosomana na
Uwezeshaji wa Biashara nchini” (Interoperability of Institutional Systems and
Business Facilitation).
Kaulimbiu hiyo, inakwenda sambamba na maagizo
na maelekezo ya Serikali ya kuhakikisha mifumo inasomana ifikapo Desemba mwaka
huu, Pia taarifa hiyo imesema kwa kuwa urasimishaji wa biashara ni mchakato ni
vema kupitia mkutano huo sekta za umma zinazoratibu urasimishaji wa biashara
nchini wakasikiliza namna bora ya sekta binafsi inavyopenda ihudumiwe kupitia
mifumo kusomana.
Taarifa
hiyo kwa vyombo vya habari nchini, imesema kwamba kutokana na uzoefu
uliopatikana katika mkutano wa kwanza wa wadau wa BRELA uliofanyika Oktoba 27,
2023 na kuhudhuriwa na washiriki wapatao 350, ulitoa mwanga na kuonesha umuhimu
wa kukutana na kukaa pamoja na wadau kila mwaka ili kubaini fursa, mafanikio na
changamoto wanazokabiliana nazo sekta binafsi.
“Mikutano kama hii kwa kiasi kikubwa inasaidia
kupata uelewa wa pamoja kuhusu namna ya kupata majawabu ya fursa, mafanikio na
changamoto na inatarajiwa katika mkutano wa mwaka huu wadau wataweza kupata
mrejesho wa majukumu yanayofanywa na BRELA ikiwemo, kupata mrejesho wa maoni.
Pia
kupata mrejesho kuhusu ushauri na mapendekezo ya wadau kwenye mkutano uliofanyika
mwaka jana, kupata mrejesho wa huduma za BRELA na kuweka mkakati wa pamoja ili
kuboresha huduma zinazotolewa na kupata maoni juu ya utendaji kazi wa BRELA
hasa matumizi ya mifumo kwa kusomana na mifumo ya taasisi zingine.
Aidha
mkutano huo utajadili mada kuhusu mifumo ya taasisi za Serikali kusoma na
uwezeshaji kibishara nchini na kubaini changamoto zinazowakabili wadau na
kuzitafutia ufumbuzi ili kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini.
Pia
utakuza uelewa wa wadau kuhusu sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza utoaji
wa huduma za usajili, ulinzi na utoaji leseni ili kuimarisha utekelezaji wa
sheria za nchi na Kujadili masuala yanayohusu maendeleo ya sekta ya biashara
nchini ikiwemo fursa zinazotokana na mabadiliko ya teknolojia na namna
yanavyochochea ukuaji wa biashara.
Mkutano
huo wa Pili wa BRELA na Wadau wake utawakutanisha wadau zaidi ya 300, wakiwemo wawakilishi
wa taasisi za umma, sekta binafsi, taasisi miamvuli, wafanyabiashara,
wanazuoni, wajasiriamali na mawakili kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini.
Aidha
utakuwa sehemu ya kubadilishana uzoefu utakaowezesha kuboresha na
kuimarisha huduma pamoja na kuongeza ufanisi na tija kwenye utoaji wa huduma na
utasaidia kutatua changamoto wanazokutana nazo wateja na wadau wa BRELA.
Taarifa
hiyo imesema mkutano huo utakaofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar
es Salaam, utaendeshwa kwa muundo wa mdahalo ambao utawezesha watoa mada,
wachagizaji na waongoza mijadala kuhusiana na mada zilizopo kuibua mjadala
kulingana na mada husika.
Washiriki
wapatao 300 wanatarajiwa kushiriki katika Mkutano huu ambapo Taasisi mbalimbali
zimeonesha nia ya kushiriki katika Mkutano kama washiriki na baadhi wakiwa
sehemu ya wadhamini.





No comments:
Post a Comment