WHI YATWAA TUZO YA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU ZAIDI AFRIKA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, October 23, 2024

WHI YATWAA TUZO YA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU ZAIDI AFRIKA


NA MAGENDELA HAMISI

WATUMISHI Housing Investments (WHI), imefanikiwa kutunukiwa tuzo ya Nyumba za Gharama nafuu zaidi Afrika ambayo imetolewa na Taasisi ya Mikopo ya Nyumba ' Africa Union for Housing Finance ' (AUHF).

Akizungumza mbele ya waandishi wa Habari, leo Oktoba 23 jijini Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa WHI, Dkt Fred Msemwa, amesema tuzo hiyo ya heshima inatambua majukumu ya taasisi hiyo katika kuwezesha umiliki wa nyumba kwa watu wa kipato cha chini.

"Pia wanatambua juhudi  tunazozifanya katika kuleta suluhisho la njia nafuu za  malipo za Nyumba ikiwemo malipo endelevu yanayolipwa kipindi cha ujenzi bila riba pamoja na utaratibu wa mpangaji mnunuzi na ndio Kuu ya kupata ushindi huo," amesema.

Ameongeza kuwa WHI ndio taasisi ya kwanza hapa Tanzania na Afrika Mashariki kupata tuzo hiyo na ni sehemu ya mafanikio katika miaka 10 tangu kuanzishwa kwa WHI na tayari wameshajenga nyumba zaidi ya 1000.

Dkt. Msemwa amesema kwamba tuzo hiyo pia heshma kwa nchi na anampongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kulahisisha kuwapa Watanzania makazi ya bei nafuu kupitia ujenzi nafuu wa nyumba hizo.

Ameongeza kwamba tuzo hiyo ni uthibitisho WA dhamira ya Serikali kupitia Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika kuwezesha wananchi kupata makazi kwa bei nafuu.

Pia ameongeza kwamba kwa Jiji la Dar es Salaam, wanaendelea na ujenzi wa nyumba 100 na Dodoma nako wanaendelea na ujenzi wa nyumba 140 ili kutimiza 1000 jijini humo.




 

No comments:

Post a Comment