NA MWANDISHI WETU
MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imeendelea kuwajengea uwezo watumishi wake katika maeneo mbalimbali ambapo kwa sasa inaendesha mafunzo maalum ya siku 5 kuanzia tarehe 5-9 Januari 2026 kwa wajumbe wa bodi ya zabuni (Tender Board) ili kuwaongezea ujuzi zaidi katika utekelezaji wa majukumu yao.
Akifungua mafunzo hayo jijini Mwanza mwenyekiti wa bodi ya zabuni wa Mamlaka hiyo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Salma Chisonga amesema mafunzo hayo kwa wajumbe wa bodi ya zabuni ni sehemu ya kuwaongezea maarifa kwa ajili ya kufanya kazi zao kwa ufanisi na kuzingatia taratibu zilizopo ili kuendelea kutoa huduma kwa wakati.
“Mafunzo haya ni sehemu ya Jitihada za Uongozi wa Shirika chini ya Kamishna wa Uhifadhi Bw. Abdul-Razaq Badru kuhakikisha kuwa makundi mbalimbali yanapata mafunzo ili kuboresha utoaji wa huduma, kuongeza ufanisi katika utendaji kazi kwa kuzingatia wakati tulionao kwa sasa) amefafaanua Kamishna Chisonga.
Kamishna Chisonga amebainisha kuwa Mamlaka hiyo imeamua kuboresha mifumo yake ya utendaji kazi kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia na kuiwezesha Ngorongoro kufikia viwango vya juu na kuwa Premium Safari Destination.
Wawezeshaji wa Mafunzo hayo ya siku 5 kutoka Taasisi ya Uhasibu Tanzania bwana Uswege İbrahim na bwana Alfred Manda wamewataka wajumbe wa bodi hiyo kuendelea kuzingatia weledi katika utendaji kazi wao ili thamani ya fedha za umma kwenye manunuzi ionekane.








No comments:
Post a Comment