Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele,
akizungumza wakati akifungua mkutano wa siku moja wa Tume na Wadau wa Uchaguzi
uliofanyika leo Novemba 29, 2024 mkoani Arusha ikiwa ni maandalizi ya
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao unataraji kuanza Disemba
11 hadi 17, 2024. Wadau hao ni pamoja na Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi
wa Dini, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Wahariri wa Vyombo vya habari,
Waandishi wa habari, Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri, Wawakilishi wa
Makundi mbalimbali ya Vijana, Watu wenye ulemavu, Wanawake na Wazee wa Kimila.
Makamu Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji wa Rufaa(Mstafu) Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifungua mkutano wa siku moja wa Tume na Wadau wa Uchaguzi
uliofanyika leo Novemba 29, 2024 mkoani Kilimanjaro ikiwa ni maandalizi ya
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao unataraji kuanza Disemba
11 hadi 17, 2024. Wadau hao ni pamoja na Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi
wa Dini, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Wahariri wa Vyombo vya habari,
Waandishi wa habari, Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri, Wawakilishi wa
Makundi mbalimbali ya Vijana, Watu wenye ulemavu, Wanawake na Wazee wa Kimila.
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji wa Rufaa(Mstafu) Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifungua mkutano wa siku moja wa Tume na Wadau wa Uchaguzi uliofanyika leo Novemba 29, 2024 mkoani Kilimanjaro ikiwa ni maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao unataraji kuanza Disemba 11 hadi 17, 2024.
Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele,
akizungumza wakati wa mkutano wa siku moja wa Tume na Wadau wa Uchaguzi
uliofanyika leo Novemba 29, 2024 mkoani Arusha ikiwa ni maandalizi ya
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao unataraji kuanza Disemba
11 hadi 17, 2024. Wadau hao ni pamoja na Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi
wa Dini, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Wahariri wa Vyombo vya habari,
Waandishi wa habari, Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri, Wawakilishi wa
Makundi mbalimbali ya Vijana, Watu wenye ulemavu, Wanawake na Wazee wa Kimila. Kulia ni Mkurugenzi wa Uchagizi wa
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Kailima Ramadhani.
Mjumbe wa Tume Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar akifuatilia mada wakati wa mkutano.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Bw. Kailima Ramadhani akiwasilisha mada ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Daftari na TEHAMA wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Bw.Stansalaus Mwita akiwasilisha mada ya Mfumo wa Uboreshaji wa Daftari katika mkutano huo. Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Daftari na TEHAMA (Daftari), Bw. Martin Mnyenyelwa akiwasilisha mada wakati wa mafunzo kwa wadau kuhusu mfumo wa uboreshaji kilichofanyika Mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Bi Giveness Aswile akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC, wakati wa mafunzo kwa wadau kuhusu mfumo wa uboreshaji kilichofanyika Mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za kisheria wa INEC, Bw. Selemani Mtibora akifafanua jambo wakati wa mkutano wa wadau mkoani Kilimanjaro.
Wadau wa uchaguzi kutoka Mkoani Kilimanjaro wakiwa mkutano wa wadau.
Wadau
wa uchaguzi kutoka Mkoani Arusha wakishiriki mkutano wa Tumen a Wadau wa
Uchaguzi ikiwa ni maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
ambao unataraji kuanza Disemba 11 hadi 17, 2024. Wadau hao ni pamoja na
Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia,
Wahariri wa Vyombo vya habari, Waandishi wa habari, Maafisa Habari wa Mikoa na
Halmashauri, Wawakilishi wa Makundi mbalimbali ya Vijana, Watu wenye ulemavu,
Wanawake na Wazee wa Kimila.
UBORESHAJI wa Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura Mkoani Arusha na Kilimanjaro utafanyika kwa siku saba kuanzia tarehe 11
hadi 17 Desemba, 2024.
Akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi mkaoni
Arusha leo tarehe 29 Novemba, 2024, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya
Uchaguzi, Jaji wa Rufaa, Jacobs Mwambegele amesema uboreshaji huo pia
utajumuisha Mkoa wa Dodoma kwenye Halmashauri za Wilaya ya Kondoa, Chemba na
Mji wa Kondoa ambapo vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na
kufungwa saa 12:00 jioni.
Amesema mikoa hiyo inafanya uboreshaji wa
Daftari ikiwa ni mwendelezo wa zoezi hilo ambalo lilizinduliwa tarehe 20 Julai,
2024 mkaoni Kigoma.
Akifungua mkutano kama huo mkoani
Kilimanjaro, Makamu Mweneyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe Jaji wa
Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk amesema zoezi hilo tayari limeshafanyika
Kigoma, Tabora, Katavi, Geita, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu,
Manyara, Dodoma, Singida na Zanzibar.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa Uchaguzi
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhan amesema Tume imeridhia
kuongezeka kwa vituo 44 vya kupigia kura ambavyo vinafanya idadi ya vituo vya
kupigia kura nchini kuwa 40,170 kutoka 40,126 vilivyokuwepo awali.
“Tume imeridhia kufanyika kwa mabadiliko ya
idadi ya vituo vya kuandikisha wapiga kura kutoka vituo 40,126 hadi kufikia
vituo 40,170 kwa kurejesha vituo 44 vya Kata 11 za Halmashauri ya Wilaya ya
Ngorongoro. Vituo 39,753 vipo Tanzania Bara na 417 vipo Zanzibar,” amesema.
Hatua hiyo ya Tume imetokana na amri ya
Waziri wa Nchi, mwenye dhamana ya TAMISEMI kupitia Tangazo la Serikali Na. 796
ya tarehe 06 Septemba, 2024 ambayo pamoja na mabadiliko mengine, imerejesha
kata 11 za Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro ambazo zilifutwa hapo awali.
Kailima amesema kwenye Mkoa wa Arusha Tume
inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 224,499 ikiwa ni ongezeko la asilimia
18 ya wapiga kura 1,255,584 waliopo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Ameongeza kuwa Tume inatarajia baada ya
uandikishaji Mkoa wa Arusha utakuwa na wapiga kura 1,480,083.
Amesema kwa Mkoa wa Arusha kuna vituo 1,454
vitakavyotumika kwenye uboreshaji kwa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la vituo 86
katika vituo 1,368 vilivyotumika kwenye uboreshaji mwaka 2019/20.
Akiwasilisha nada mkoani Kilimanjaro,
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume, Selemani Mtibora amesema kwa mkoa
wa Kilimanjaro Tume inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 180,540 ikiwa ni
ongezeko la asilimia 18 ya wapiga kura 1,009,726 waliopo kwenye Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura.
“Tume inatarajia baada ya uandikishaji Mkoa
wa Kilimanjaro utakuwa na wapiga kura 1,190,266,” amesema.
Ameongeza kuwa Mkoa wa Kilimanjaro una vituo
1,316 vitakavyotumika kwenye uboreshaji kwa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la
vituo 30 katika vituo 1,286 vilivyotumika kwenye uboreshaji mwaka 2019/20.
Wadau
wa uchaguzi kutoka Mkoani Arusha wakishiriki mkutano wa Tumen a Wadau wa
Uchaguzi ikiwa ni maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
ambao unataraji kuanza Disemba 11 hadi 17, 2024. Wadau hao ni pamoja na
Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia,
Wahariri wa Vyombo vya habari, Waandishi wa habari, Maofisa Habari wa Mikoa na
Halmashauri, Wawakilishi wa Makundi mbalimbali ya Vijana, Watu wenye ulemavu,
Wanawake na Wazee wa Kimila.
No comments:
Post a Comment