NA MWANDISHI WETU
ITEL Mobile, chapa maarufu ya simu za mkononi duniani kwa ushirikiano na Airtel Tanzania, mtandao mpana na wenye kasi imezindua simu yake mpya ya kisasa Itel A80.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 12, 2024 Wakati wa uzinduzi huo, Meneja Masoko na Mahusiano wa Itel, Sophia Msafiri amesema simu hiyo ya Itel A80 inakuja na muundo wa kisasa na sifa bora zinazowafanya watumiaji wake kufurahia matumizi ya kipekee.
"Itel A80 inajivunia skrini kubwa ya Nchi 8.7 yenye punch-hole, betri yenye uwezo wa 5000mAh inayodumu muda mrefu na kamera ya 13MP yenye ubora wa hali ya juu kwa picha na video.
"Pia, simu ya Itel A80 ina nafasi kubwa ya kuhifadhi data GB 128 + GB 8, kuhakikisha watumiaji Wana uhuru wa kuhifadhi maudhui yao kwa urahisi. Simu hizi zitapatikana katika maduka yetu yote Nchi nzima kwa gharama nafuu kwa mkopo au kwa kulipa pesa taslimu," amesema.
Kwa upande wake Meneja Mahusiano wa Airtel Tanzania, Jennifer Mbuya amesema kupitia ushirikiano huo, wateja wa Airtel watapata ofa Maalum itakayowawezesha kufurahia huduma za intaneti kwa gharama nafuu wanapokuwa na Itel A80, hivyo kuboresha zaidi matumizi yao hasa kipindi hiki cha msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.
Kwamba uzinduzi wa wa Itel A80 unaonyesha ari ya Airtel Tanzania katika kupunguza mgawanyiko wa kidigitali nchini kupitia Teknolojia suluhishi kwa bei nafuu.
"Ushirikiano Wetu na Itel utaongeza matumizi ya simu kwa watumiaji wa Airtel kote nchini kwa kuchanganya vipengele vya kisasa vya Itel na mtandao Bora wa Airtel wenye kasi zaidi. Ushirikiano huu unaonyesha jinsi tunavyojitolea katika kurahisisha maisha ya wateja Wetu kupitia bidhaa za ubunifu," amesema.






No comments:
Post a Comment