RC CHALAMILA ATEMBELEA KIWANDA CHA SUMA JKT SKYZON - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, November 12, 2024

RC CHALAMILA ATEMBELEA KIWANDA CHA SUMA JKT SKYZON


NA MWANDISHI WETU

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amewataka viongozi mkoani humo ikiwemo wakuu wa wilaya,wakurugenzi wa halmashauri na wakandarasi kutoka TARURA na TANROAD kutumia kiwanda cha taa cha SUMA JKT ili kupata taa bora zitakazowekwa katika jiji hilo na kuwezesha  watu kufanya kazi usiku na mchana


RC Chalamila ameyasema hayo leo Novemba 12,2024  alipotembelea kiwanda cha taa kinachomilikiwa na SUMA JKT kilichopo Mlalakua Wilaya ya  kinondoni ambapo pamoja na kuridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na jeshi hilo la kujenga Taifa ameagiza kiwanda hicho kitumike kama suluhisho la upatikanaji wa taa bora jijini humo.


Aidha RC Chalamila amewataka viongozi wa Mkoa huo kutumia kiwanda hicho kupata taa bora za kuweka maeneo mbalimbali ikiwemo barabarani na kwenye masoko kuwezesha biashara zifanyike usiku na mchana huku pia akitaka maabara ya kiwanda hicho kutumika kufanya majaribio ya taa zinazoingizwa kutoka nje ya nchi


Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT Brigedia Jenerali Petro Ngata amesema kiwanda hicho kinchojulikana jina la SUMA JKT SKYZON kinatengeneza taa za LED zinazotumia umeme na mfumo wa Solar na kwamba kwa ukanda wa Africa Mashariki hicho ni kiwanda cha kwanza kinachotengeneza taa bora na kinatarajia kuzinduliwa hivi karibuni hivyo amewataka wadau kutumia kiwanda high kupata taa


Pia, RC Chalamila ametoa rai kwa watumishi wanaofanya kazi katika kiwanda hicho kufanya kazi kwa bidii pamoja na kuwa na uaminifu aidha kiwanda hicho kwa sasa kimesha anza uzalishaji na kinatarajiwa kufunguliwa raasmi hivi karibuni.




No comments:

Post a Comment