NIMEPIGA KURA; NIMETIMIZA HAKI YANGU YA KIKATIBA- KAPINGA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, November 27, 2024

NIMEPIGA KURA; NIMETIMIZA HAKI YANGU YA KIKATIBA- KAPINGA


NA MWANDISHI WETU, RUVUMA

NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga leo ameshiriki zoezi la kupiga kura katika Kitongoji cha Mheza kijiji cha Mkumbi Halmashauri ya Mbinga Vijijini ili kuchagua viongozi wa eneo husika.


Kapinga ameeleza kuwa, kwa kufanya hivyo ametimiza haki yake ya kikatiba na kutoa wito kwa Watanzania wote kuitumia haki hiyo kikamilifu.


Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni miongoni mwa mihimili muhimu ya demokrasia inayowezesha ushiriki wa wananchi katika uongozi wa maeneo yao.





No comments:

Post a Comment