TUTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA WADAU KUIMARISHA SEKTA YA AFYA NCHINI – MAJALIWA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, November 21, 2024

TUTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA WADAU KUIMARISHA SEKTA YA AFYA NCHINI – MAJALIWA



NA WAF 

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa  amesema Serikali  ya Jamhruri ya Muungano wa Tanzania na ya  Mapinduzi ya Zanzibar zitaendelea kushirikiana na  wadau pamoja na taasisi zote za afya  ili kuhakikisha kuwa huduma za afya zinaimarika ikiwa ni pamoja na kukabiliana na dharura za kiafya.


Aidha ametoa kauli hiyo Novemba 21, 2024 wakati wa hafla ya uzinduzi wa ripoti ya mapitio ya hali ya utekelezaji wa Afya kwa wote na utayari wa kukabiliana na dharura nchini lililofanyika jijini Dar es Salaam.


Pia amewashuruku wadau wote kwa ushirikiano wanaoutoa kwa Serikali  zote mbili na kwamba  zinathamini mchango wao na zitaendelea kuunga mkono katika yale ambayo  wadau hao pia wanaunga mkono hasa katika mkakati wa Serikali wa utekelezaji wa afya kwa wote na utayari dhidi ya dharura.

“Ninatoa pongezi kwa timu ya wataalamu ambayo imefanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kuwa taarifa ya hali ya utekelezaji wa afya kwa wote  pamoja na utayari dhini ya dharura inapatikana na kuwasilishwa kwa ajili ya kujadiliwa, nina imani itakwenda kuleta maslahi kwa nchi,” amesema Mhe. Majaliwa.


Amesema mjadala huu utarahisha utekelezaji wa vipaumbele vya  afua zote muhimu katika utekelezaji wa shughuli za Serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya. Vilevile itakuwa fursa kwa wadau kuelewa maeneo yanayofanya vizuri na yale yenye changamoto ili Serikali iweze kuyapatia ufumbuzi.

Majaliwa amesema Serikali  ina imani kuwa  uzinduzi wa ripoti hiyo utaweka mikakati itakayokwenda sambamba  na maazimio ya kimataifa  chini ya Shirika la Afya Duniani (World Health Organization-WHO) katika mkutano wa 73 wa Afya Duniani uliofanyika mwaka 2020  kuhusu utekelezaji wa  hiari wa mapitio shirikishi  wa hali ya utekelezaji wa afya kwa  wote na utayari dhidi ya dharura za kiafya kwa nchi wananchama wa WHO.


Awali akizungumza  katika hafla hilo Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amesema Serikali  ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imewezeka  kwa kiasi kikubwa katika sekta ya Afya kwani fedha zaidi ya Shilingi Trilioni 6.2 zimetumika katika kuimarisha sekta ya afya ndani ya miaka mitatu.


Amesema kutokana na uwekezaji huu  Bima ya Afya kwa wote itakuwa ni muarobaini kwa kuhakikisha Watanzania wananufaika na uwekezaji huo kwa kupata huduma za afya wakiwemo walio na vipato duni kutokana na jitihada zinazofanywa na Serikali za kutenga fedha kwa ajili ya kundi hilo.


“Kwa mwaka wa Fedha 2023/2024 Serikali imetenga fedha kiasi cha TZS Bilioni 173 kwa ajili ya kuwapatia huduma za afya wananchi wasio  na uwezo ambao ni sawa na asilimia 26 ya Watanzania wote, hizi ni Jitihada za dhati zinazofanywa na Serikal  katika kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata huduma za Afya, amefafanua Mhe. Mhagama.


Hafla ya uzinduzi wa repoti hiyo umeratibiwa na ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Wizara ya Afya pamoja na ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa ushirikiano na WHO na wadau mbalimbali wa sekta ya Afya kutoka ndani  na nje ya Tanzania.







No comments:

Post a Comment