Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Kampuni ya Simu ya Airtel Tanzania, Jackson Mmbando. akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Promosheni ya Airtel Santa Mizawadi uliofanyika makao makuu ya Airtel Tanzania jijini Dar es Salaam, Desemba 17, 2024.Kushoto ni Meneja Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Celina Njuju.
…………………………..
NA DOTTO MWAIBALE
KAMPUNI ya
Simu ya Airtel Tanzania inaanza msimu huu wa sikukuu na Airtel Santa Mizawadi kupitia promosheni maalum yakutoa shukrani na
kuwazadia wateja na mawakala wote wanaoendelea kutumia huduma za Airtel katika
msimu wa sikukuu.
Akizungumza
wakati wa hafla ya uzinduzi wa promosheni hiyo ya Airtel Santa Mizawadi iliyofanyika makao makuu
ya Airtel Tanzania jijini Dar es Salaam Desemba 17, 2024, Mkuu wa Mawasiliano
na Uhusiano, Jackson Mmbando alisema Promosheni ya Airtel Santa Mizawadi
inalenga kuwashukuru wateja na mawakala waaminifu na wanaoendelea kutumia
Airtel katika msimu wote huu wa sikukuu.
“ Airtel
Santa Mizawadini promosheni kabambe ambayo itawapa washindi fursa ya kuondoka
na zawadi kemkem ikiwemo pocket WiFi, simu janja, pikipiki, runinga na pesa
Taslim hadi shilingi milioni moja, “ alisema Mmbando.
Akielezea jinsi ya kushiriki na kujishindia Mizawadi ya Airtel Santa Mizawadi, Mmbando alisema ikiwa wewe ni Wakala wa Airtel unatakiwa tu kufanya miamala ya kuweka na kutoa fedha, ambapo pia ili mteja aweze kuingia kwenye droo anatakiwa tu kufanya miamala kama vile kununua bando, Kutuma pesa, kutoa pesa, kulipa bili, kufanya miamala ya kibenki, kutuma au kupokea pesa nje ya nchi, kununua muda wa maongezi au vifurushi kupitia *149*99#, *150*60#, au kwa kutumia ‘My Airtel App’.
Kwa upande
wake Meneja Huduma kwa Wateja, Celina Njuju alisema kampuni hiyo inawathamini
sana wateja wake wote hivyo wachangamkie fursa ya kupata mizawadi kupitia
promosheni hiyo kama ilivyoelezwa na Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano, Jackson
Mmbando.
Njuju
alisema kila wiki watachezesha droo kwa ajili ya kuwapata washindi na kuwa
washindi hao watapigiwa simu kupitia namba 100 kama ambavyo wamekuwa
wakiwasisitizia wateja wao kutotoa taarifa zao kwa mtu mwingine yeyote bali kwa
kutumia namba hiyo.
Aidha Njuju alisema Promosheni hiyo itanogeshwa na Balozi wao Mr Santa ambaye atakuwa akipita mitaani na kuwa watakapokutana naye anawahakikishia kuwa siku yao itanogeshwa zaidi na zaidi na balozi huyo.
Meneja Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Celina Njuju, akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi huo.
Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Kampuni ya Simu ya Airtel Tanzania, Jackson Mmbando na Meneja Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Celina Njuju wakijadiliana jambo wakati wa uzinduzi huo.
Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Kampuni ya Simu ya Airtel Tanzania, Jackson Mmbando, akionesha moja ya bidhaa zitakazotolewa kama zawadi kwa washindi. Kushoto ni Meneja Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Celina Njuju.
No comments:
Post a Comment