NA MWANDISHI WETU
MWANA
DADA Fatuma Mwandege mkazi wa Majumba Sita Ukonga, jijini Dar es Salaam
amefanikiwa kuandika historia kwa kutwaa pikipiki katika wiki ya kwanza ya
promosheni ya Santa Mizawadi.
Katika
droo ambayo imechezeshwa leo Desemba 24, 2024 na Meneja Mahusiano wa Kampuni
hiyo, Jackson Mmbando, pia zawadi ya Runinga inchi 55, imekwenda kwa Halima
Kimaro akiwa mkoani Shinyanga.
Andrew Chiomo ambaye ni mwendesha Bodaboda, mkazi
wa Ifakara mkoani Morogoro, amefanikiwa kuondoka na kitita cha Shilingi Mil. 1,
zawadi ya Router kutoka Airtel ya kiwango cha 5G imechukuliwa na Josephine Mgagula
mkazi wa Nzega Tabora.
Pia
zawadi ya simu ya mkononi aina ya SmartPhone imekwenda kwa Omari Ramadhani
mkazi wa Shinyanga.
Mmbando
akizungumza katika droo hiyo ya wiki ya kwanza ya promosheni ya Santa Mizawadi
ambayo inaendeshwa na Airtel Tanzania katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Christimas,
amesema huo ni mwanzo zawadi nyingi zinakuja.
Droo
hii inafanyika kila Jumanne ya wiki kwa lengo la kuwapa wateja wetu zawadi
mbalimbali ikiwemo fedha, pikipiki, runinga, smartphone kwa wale ambao
wanatumia huduma zetu kwa njia tofautitofauti.
Mmbando
amefafanua kuwa ili wakala, mteja na mtumiaji wa huduma za kampuni hiyo
wanaingia katika promosheni hiyo kwa
wananafanya
miamala kila wiki kwa ajili ya Sikukuu ya Christmass kwa kutuma na kupokea
pesa, kulipia bili mbalimbali utaweza kujishindia na kujipatia zawadi kutoka
kwa Mr. Santa.
Ameongeza
kuwa Promosheni ya Airtel Santa Mizawadi inalenga kuwashukuru wateja na
mawakala waaminifu na wanaoendelea kutumia Airtel katika msimu wote huu wa
Sikukuu.
Akielezea
jinsi ya kushiriki na kujishindia Mizawadi ya Airtel Santa Mizawadi, Mmbando
amesema Kwa Wakala wa Airtel anatakiwa kufanya miamala ya kuweka na kutoa fedha
na Kwa mteja anachotakiwa kufanya kununua bando, kulipa bili, kutuma na kutoa
fedha, kununua muda wa maongezia au vifurushi kupitia *149*99#, *150*60# au
kupitia 'My Airtel App'.
Ameongeza kuwa washindi wote watafikishiwa zawadi
popote walipo baada ya taratibu kukamilika.
No comments:
Post a Comment