BAADA ya wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kusubiri kwa muda mrefu Shangwe la porini, jana Disemba 15, 2024 Pori la Akiba Pande lilifanikiwa kumaliza Kiu ya Jiji kupitia Samia Bash.
Kupitia burudani na shughuli za uhifadhi mbalimbali zinazopatikana Pori la Akiba Pande zilifurahiwa na wageni mbalimbali walioshiriki na kujiburudisha katika mandhari tulivu na salama, nyamapori ya kutosha, vinywaji aina zote, burudani ya kipekee kutoka bendi ya Twanga Pepeta wakali wa jiji na kujionea wanyamapori lukuki.
Miongoni mwa wageni mbalimbali waliofika ni pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule alieambatana na kamati ya ulinzi na usalama wilaya na Katibu mwenezi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Dar es Salaam Bw. Ally Bananga.
Aidha wakati wananchi wakiendelea kufurahia siku hiyo mkuu wa pori hilo Mhifadhi Mkuu P F. Massawe alisema, "Hakika tunashukuru kwa mwitikio mkubwa wa wananchi, wanaendelea kufurahi sana na wameomba tuendelee kusimamia na kushirikiana na wadau mbalimbali katika kumuunga mkono Raisi wetu Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kukuza shughuli za utalii nchini na kuwafanya wananchi wafurahie matunda ya uhifadhi."
Wananchi wameahidi kuendelea kutembelea pori hilo wakati wote kwa ajili ya kuendelea kufurahia mazingira mazuri na huduma zinazopatikana ndani ya Pori la Akiba Pande.
No comments:
Post a Comment