NA MWANDISHI WETU
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema anatarajia kufanya mazungumzo na Halmashauri ya Jiji na Shirika la Reli (TRC) kujadili uwezekano wa kujenga reli za ndani mkoani humo.
Amesema lengo la majadiliano hayo ni kuhakikisha reli inajengwa kupitia makusanyo ya kodi ya mkoa huo na ikiwa mchakato huo utakamilika itafanikisha kupunguza adha ya usafiri mkoani humo.
"Naamini tukikaa na Wadau mbalimbali wakiwemo TRC na Halmashauri ya Jiji kujadili suala hili tunaweza kupata majibu sahihi ya gharama ya ujenzi huo wa reli na tutatumia makusanyo ya kodi kufanikisha ujenzi huo," amesema.
Amebainisha hayo Januari 30, mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari ambapo pia alimshukuru Rais Samia kwa kufanikisha Mkutano wa Nishati kwa nchi za Afrika na Marais zaidi ya 20 waliudhuria.
"Namshukuru Rais Samia kwa kufanikisha mkuu huo mkubwa ambao kwa kiasi kikubwa umeitangaza nchi na Mkoa wa Dar es Salaam kwa ujumla," amesema
Wakati huo huo, Chalamila ametangaza rasmi kuanza kwa shughuli za biashara kwenye jiji hilo saa 24 ambapo uzinduzi rasmi utafanyika Februari 22 mwaka huu kwani jiji hilo ni muhimu kwenye ukuaji wa uchumi.
No comments:
Post a Comment