TUTAENDELEA KUWAUNGA MKONO DKT SAMIA, DKT MWINYI - NGWENJE - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, January 31, 2025

TUTAENDELEA KUWAUNGA MKONO DKT SAMIA, DKT MWINYI - NGWENJE


NA MWANDISHI WETU

WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikielekea kuadhimisha miaka 48 Feb 5, mwaka huu, Mwenyekiti wa Taasisi ya Furahika kinachosimamia Chuo Cha Ufundi Furahika Veta, Ngwenje Mohamed, amesema wataendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt Husseni Alli Mwinyi.

Akizungumza na waandishi wa habari Januari 30 mwaka huu jijini Dar es Salaam, Ngwenje amesema CCM kuadhimisha miaka 48 tangu kuasisiwa kwake, Taasisi ya Furahika inatembea kifua mbele kwa kufanikisha kutoa elimu bure kwa wanafunzi zaidi ya 1500.

“Wengi wa wanafunzi ambao wamehitimu katika chuo hiki wamefanikiwa kupata ajira katika maeneo mbalimbali nchini na hayo ni mafanikio ambayo  tunavUnia kupitia miaka 48 ya Chama Cha Mapinduzi CCM na kwa muktadha huo tutaendelea kikiunga mkono CCM kutokana na usimamizi mzuri wa sera ya elimu,” amesema.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiliasisiwa Mei 5, 1977 baada ya kuunganishwa kwa vyama vya Tanganyika Africa National Union (TANU) kilichokuwa kikitawala Tanzania Bara chini ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere  na Afro Shirazi Party (ASP), kilichokuwa kikiongozwa na Hayati Sheikh Amaan Abeid Karume aliyekuwa rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

 “Ngwenje pia amewapongeza wajumbe wa  mkutano Mkuu wa CCM kwa kumchagua Dkt Samia kuwa ajili ya uchaguzi Mkuu wa ujao, akiamiani kuwa haikuwa kwa bahati bali ni kutokana na uchapakazi mzuri ambao ameuonesha katika kipindi chake cha uongozi wa miaka minne tangu aingie madarakani,” amesema.

Akizungumzi uelekeo wa chuo chake katika kufikia mafaniko Ngwenje amesema kwa sasa wanajipinga kufikia Mei mwaka huu kila mwanafunzi atakayejiunga na chuoni hapo atakuwa akipata chakula bure ili kumweka sawa kiakili jambo litakalofanya kufanya vizuri zaidi katika masomo.

Kulingana na hilo ametoa wito kwa wazazi kuendelea kupeleka vijina wao ambao wameshindwa kuendelea na elimu kwa vikazo mbalimbali ikiwemo fedha au kutofanya vuzri kidato cha nne ama cha pili au darasa la sana, wao watamuendeleza kielimu bure kupitia mradi wa Elimu Bure wenye lengo la kuwaondoa vijana katika dimbwi la umasikini kutokana na ukosefu wa ajira.

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment