MVUA KUBWA ZINATARAJIA KUWEPO KWA MUDA MFUPI - TMA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, January 23, 2025

MVUA KUBWA ZINATARAJIA KUWEPO KWA MUDA MFUPI - TMA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Mwakilishi wa Kudumu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Dkt. Ladislaus Chang'a akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.


NA MWANDISHI WETU

MVUA kubwa zinatarajiwa kunyeesha kwa muda mfupi katika maeneo yote yanayopata mvua za wastani hadi juu ya wastani katika kipindi hiki cha mvua za masika zinazotarajiwa kuanza katika wiki ya kwanza ya mwezi  Machi mwaka huu na kutamatika Mei, mwaka huu.

Hayo yamebainishwa leo Januari 23, 2025 jijini, Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Ladislaus Chang'a wakati akitoa mwelekeo wa mvua za msimu wa Masika zitakazoanza Machi hadi Mei 2025 kwa maeneo yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka.

 

“Matukio ya mvua kubwa ya wastani zinaweza kujitokeza kwa muda mfupi katika maeneo yote yanayopata mvua za wastani na juu ya wastani na kuweza kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi na uharibifu wa miundombinu, mazingira, mlipuko wa magonjwa  na upotevu wa mali.

“Hivyo , mamlaka husika katika Idra ya Menejimenti ya Maafa kwa kushirikiana na wadau tunawashauri kuendelea kuendelea kuratibu utekelezaji wa mipango itakayosaidia kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza, amesisitiza.

Dkt. Chang'a ambaye pia ni Mwakilishi wa Kudumu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, amesema kwamba mvua za wastani hadi chini ya wastani zinarajiwa kunyeesha katika maeneo ya Pwani ya Kaskazini, Kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma na Ukanda wa Ziwa Victoria.

 

Pia amesema mvua za wastani hadi juu ya wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki pamoja na Mashariki mwa Mikoa ya Mara na Simiyu.

 

Aidha ameongeza kuwa mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa kuwepo katika maeneo ya Pwani ya Kaskazini, Kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma na Ukanda wa Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga na magharibi mwa mikoa ya Simiyu na Mara) katika kipindi cha Msimu wa Masika, 2025,”.

 

Ameongeza kuwa, ongezeko la mvua linatarajiwa katika kipindi cha mwezi Aprili 2025, ambapo ametoa angalizo la matukio ya hali mbaya ya hewa ikiwemo vipindi vya mvua kubwa kujitokeza hata katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za Wastani hadi Chini ya Wastani.

 

Kuhusu athari zinazoweza kujitokeza, Dkt. Chang’a amesema Mvua za Wastani hadi Chini ya Wastani zinazotarajiwa katika baadhi ya maeneo zinaweza kupelekea upungufu wa upatikanaji wa maji kwa matumizi ya majumbani, ufugaji na kilimo.

 

MWISHO


NA ABRAHAM NTAMBARA 

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa mwelekeo wa mvua za msimu wa Masika Machi hadi Mei 2025 kwa maeneo yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 23, 2025 jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Mwakilishi wa Kudumu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, Dkt. Ladislaus Chang'a amesema mvua za wastani hadi juu ya Wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki pamoja na Mashariki mwa mikoa ya Mara na Simiyu.

Dkt. Chang'a ameongeza kuwa mvua za wastani hadi chini ya wastani zinarajiwa katika maeneo ya Pwani ya Kaskazini, Kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma na Ukanda wa Ziwa Victoria.

“Mvua za wastani hadi juu ya wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki pamoja na Mashariki mwa Mikoa ya Mara na Simiyu," amesema Dkt. Chang'a na kuongeza,

"Aidha, mvua za Wastani hadi Chini ya Wastani zinatarajiwa katika maeneo ya Pwani ya Kaskazini, Kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma na Ukanda wa Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga na magharibi mwa mikoa ya Simiyu na Mara) katika kipindi cha Msimu wa Masika, 2025,”.

Ameongeza kuwa, ongezeko la mvua linatarajiwa katika kipindi cha mwezi Aprili 2025, ambapo ametoa angalizo la matukio ya hali mbaya ya hewa ikiwemo vipindi vya mvua kubwa kujitokeza hata katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za Wastani hadi Chini ya Wastani.

Kuhusu athari zinazoweza kujitokeza, Dkt. Chang’a amesema Mvua za Wastani hadi Chini ya Wastani zinazotarajiwa katika baadhi ya maeneo zinaweza kupelekea upungufu wa upatikanaji wa maji kwa matumizi ya majumbani, kilimo na ufugaji.

No comments:

Post a Comment