DKT MSUYA 'AWANG'ATA SIKIO' WAKUU VYUO VYA UFUNDI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, January 6, 2025

DKT MSUYA 'AWANG'ATA SIKIO' WAKUU VYUO VYA UFUNDI


 
NA MWANDISHI WETU

UONGOZI wa Chuo cha Ufundi cha Furahika ambacho kipo Buguruni Malapa, Ilala jijini Dar es Salaam umetoa wito kwa wakuu vyuo vya ufundi nchini kuajiri walimu wenye taaluma ya kufundisha watu wenye mahitaji maalumu.

Chuo hicho ambacho kipo  chini ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Aprili mwaka huu kimejipanga kuanza kwa vitendo kuajiri walimu wa lugha ya alama ili kusaidia kufundisha wanafunzi wenye mahitaji maalumu wakiwemo wasiona na viziwi.

Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Dkt David Msuya amebainisha hayo, jijini Dar es Salaam, leo Januari 6, 2025 alipozungumza na waandishi wa habari na kufafanua kuwa ikiwa vyuo vingi vitakuwa na walimu wa kufundisha wenye mahitaji maalumu itasaidia Serikali kutimiza ndoto ya watu kundi hilo kupata elimu ya Ufundi na kuwaondoa katika janga la ukosefu wa Ajira.


Pia amesema ili kuzingatia utawala bora na haki ya kusoma ya kila mtanzania bila aliye na hasiye na ulemavu kuwa na miundombinu rafiki mahali pa kutoa elimu ni jambo la msingi ili kuweka usawa kwa wote. 

"Msiweke madarasa yenye ngazi kwaajili ya watu wenye ulemavu hasa ya wale wanaotambaa au wanaotembea kwa njia ya baiskeli, wanashindwa kuingia darasani kwa sababu ya madarsa mengi yamekuwa na ngazi" Amesema Dkt. Msuya

Amesema serikali na taasisi nyingine zinapoandaa miradi ya elimu kuzingatia kujenga miundombinu itakayowawezesha walemavu kuitumia.

Amesema kuwa vyuo viwe na walimu wa lugha za alama ili kuwatendea haki watu wenye ulemavu kwenye vyuo na kuwafanya walemavu wote kupata elimu sawa na wanafunzi wengine ambao hawana ulemavu.

"Niipongeze wizara ya elimu imejitahidi sana kwani inayowalimu wengi wanaofundisha lugha za alama, 2025 Vyuo tubadilike tutafute walimu, wawepo kila idara ili tutimize ndoto za serikali za awamu ya sita kupitia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani, nia yake ni njema sana lakini taasisi hizi za elimu tunatakiwa tujiongeze sisi wenyewe kuona kwamba tunawainua watu wenye mahitaji maalumu." Amesema

Amesema kuwa Chuo Chake wamefanikiwa kupata walimu wa watu wenye ulemavu wawili, pia amewaomba vyuo vingine walifanye jambo hili ili watanzania wenye ulemavu wawe na haki sawa kama walivyo wengine kwa kupata elimu na ujuzi.

Pia amesema kuanzi Aprili, 2025 katika chuo hicho wanatarajia kuanzisha fani ya ushonaji viatu pamoja na kazi ya uhudumu kwenye magari kwani kunawatu wanausafiri wa mabasi lakini hakuna wahudumu.

Pia amesisitiza kuwa soko la ajira lisichague aina ya watu, wenye ulemavu na wasio na ulemavu kwaajili ya kufanya kazi, waajili watu wote.

"Ulemavu unaweza kumkuta mtu yeyote kwahiyo soko la ajira lisichague ili kila mmoja anufaike na mirafi mbalimbali inayoanzishwa na serikali." Amesema Dkt. Msuya.


"Ili kupunguza unyanyapaai na kutende haki pande zote mbili tutende haki kwa walemavu wa mikono, wa miguu, macho na viziwi kwani, wanahaki ya kupata mafunzo ya veta ili watimize malengo yao na tujiongeze kubadilishane ujuzi kutoka vyuo tofauti tofauti." Amesema Dkt. Msuya

Licha ya hayo Dkt. Msuya pia amewakaribisha Watoto wote waliopo mtaani, waliofeli darasa la Saba na kidato cha nne kuanzia mwaka 2022 mpaka sasa kujiunga na chuo hicho kwani mpaka sasa kinanafasi 400 za kujiunga.

Na fomu za usajili zinapatikana katika tovuti ya chuo hicho ya www.furahika.co.tz.

Wanafunzi wote kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani wanakaribishwa kujiunga na chuo hicho kwani elimu inayotolewa ni bure na haina gharama yeyote na baada ya kuhitimu katika chuo hicho watatafutiwa kazi kwani chuo hicho kinamikakati ya kufuatilia wahitimu.

No comments:

Post a Comment