Picha kwa hisani ya Mtandao
ASKARI wa Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa kushirikiana na wenzao wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Jeshi la Polisi Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, wamemuua fisi katika Kijiji cha Kimali ambaye alikuwa akiwasumbua wakazi wa eneo hilo.
Fisi huyo aliyeuawa anadaiwa kuwa na alama ya jina la mtu upande wa paja lake la kushoto, huku akiwa na shanga shingoni.
Kufuatia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Anna Gidarya amewataka wananchi wote wilayani humo wanaomiliki nyara za Serikali kinyume cha sheria kuzisalimisha haraka kwa wahusika wa uhifadhi, kabla ya hatua kali hazijachukuliwa dhidi yao.
Kumekuwepo na matukio ya fisi kushambulia watoto kuanzia majira ya saa moja usiku katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Itilima.
Takwimu zilizotolewa wilayani Itilima zinaonyesha kuwa kuanzia mwaka 2024 hadi sasa watu nane wamefariki dunia baada ya kushambuliwa na fisi na wengine 17 wamejeruhiwa, huku fisi 16 wakiuawa katika kipindi hicho.
No comments:
Post a Comment