NA MWANDISHI WETU
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imekagua miradi ya ikiwemo ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji Kibaha iliyogharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.1.
Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Kibaha, Catherine Saguti kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashari wakati akitoa taarifa juu ya ujenzi wa hospitali hiyo.
Dk Saguti amesema kuwa mapokezi ya fedha za mradi wa Ujenzi wa Hospitali na ununuzi wa vifaa tiba kutoka Serikali Kuu yalitolewa kwa awamu nne jumla ya shilingi bilioni 3.3 kwa ajli ya ujenzi na sh. milioni 400 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba.
Pia kamati hiyo imetembelea ujenzi wa kituo cha afya cha Kata ya Pangani kilichogharimu kiasi cha sh. milioni 914 huku Halmashauri ya Mji Kibaha ikichangia kiasi cha shilingi milioni 189 kutokana na mapato ya ndani.
Wabunge hao wa Kamati ya Tamisemi walitembelea mradi wa shule mpya ya Sekondari ya Kata ya Tangini iliyogharimu kiasi cha shilingi milioni 528.9.
Katika hatua nyingine kamati hiyo ya kudumu ya Bunge ya Tamisemi pia ilitembelea ujenzi wa Shule ya Msingi Mtakuja Kata ya Pangani ambayo ina mfumo wa Kiingereza ambayo imegharimu kiasi cha shilingi milioni 309.
No comments:
Post a Comment