NA MWANDISHI WETU, SINGIDA
ZAIDI ya Walimu 1500 wa Mkoa wa Singida wamefikiwa na Kliniki ya Samia ya Walimu ya kutatua changamoto zao.
Ziara ya kutatua changamoto za walimu inaratibiwa na Chama cha Walimu (CWT) kwa kushirikiana na Serikali katika kuwafikia Walimu kutoa changamoto za madai yao kwa ajili ya Serikali kufanyia kazi.
Akizungumza wakati akifungua Kliniki ya Walimu Mkoa Singida Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendegu amesema kuwa Kliniki ya Samia ya Walimu inakwenda kutatua changamoto ya madai ya Walimu.
Amesema kuwa Kliniki ya Walimu kuanzishwa kwake ni matokeo ya Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kutambua mchango wa Walimu hivyo wanahitaji kutatuliwa kwa kulipa madai yao.
Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa Walimu wa Mkoa wa Singida wamejitoa sana katika kufundisha licha ya kuwa na madai na kufanya Mkoa kuendelea kufanya vizuri katika elimu.
Ofisa Utumishi Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Judith Abdallah amesema wamejipanga katika kutatua changamoto za Walimu katika Kliniki ya Samia na kuleta matokeo.
Amesema kuwa walimu wamejipanga kutoa huduma kwa idadi iliyofika huku akidai madai mengine ni maelekezo.
Makamu wa rais wa Chama cha Walimu (CWT) Seleman Ikomba emesema zoezi la kutatua changamoto za walimu ni endelevu .
Amesema kuwa Chama kimejipanga kushirikiana na serikali katika kufanya utatuzi wa madai ya walimu hivyo hawatakubali atokee mtu kuhujumu.
Aidha amesema katika kipindi hiki watashughulika na wahujumu ambao ni walimu katika kuweka utulivu huku serikali ikifanya mchakato wa ulipaji wa madai yao.
Walimu wakiwa katika Kliniki ya kutatua changamoto yao iliyoratibiwa na CWT kwa kushirikiana na Serikali.Baadhi ya walimu wakipata huduma katika dawati la maafisa Utumishi katika Kliniki ya Samia ya kutatua changamoto za Walimu iliyofanyika Mkoa wa Singida.
No comments:
Post a Comment