Mwenyekiti wa TLP, Richard Lymo, akizumgumza (Picha kwa hisani ya mtandao).
MWENYEKITI
wa Tanzania Labour Party (TLP) Richard Lymo, amesema hayuko tayari kuungana na vyama
vingine vya siasa vya upinzani katika Uchaguzi Mkuu ujao kama chama chake
hakitapewa nafasi ya kutoa mgombea wa urais.
Lymo ameweka
wazi hayo leo, jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari waliofika
ofisini kwake kwa lengo la kutaka kujua kama chama chake kitakuwa sehemu ya
kuungana na kwa lengo la nguvu ya pamoja katika uchaguzi huo unaotarajiwa
kufanyika baadaye mwaka huu.
“Kama
watataka tuungane nitawaeleza kwamba wakipe nafasi chama changu kitoe mgombea
wa urais na si vinginevyo na ikiwa watakubali hakutakuwa na shida ila hatuwezi
kuingia kwenye mtego wa kufanya chama kingine kiwe kikubwa.
“Ebu angalia
Chama Cha Wananchi - (CUF), marehemu Maalim Seif Sharif Hamad wakati ule
aliingia kwenye UKAWA angalia kilichotokea, CUF hii si ile kwani wakati
wanaingia katika muunganiko huo hawakuangalia luzuku itakuwawaje,” amesema.
Amefafanua
kwamba Chama siku zote kinajengwa na luzuku hivyo unapoungana unafanya kimoja
kiwe kikubwa kutokana na kusikika katika uchaguzi huo na vinaweza kupata idadi
kubwa ya wabunge, madiwani na vingine vififia
na kuvinyanyua ni kazi kubwa kwa maana
kuviendesha inahitaji luzuku.
Pia alisema
wakati wa UKAWA, Wenyeviti wa Chama walikubaliana wasiingiliwe katika majimbo
yao, ingawa cha kushangaza mmojawapo aliwekewa mgombea kwenye jimbo lake kitu ambacho
alifafanua kilikuwa kinyume cha makubaliano.
Lymo,
anaamini kwamba muungano huo ambao tayari baadhi ya viongozi wa vyama upinzani
wameanza kuugusia wakiamini ndio mwarobaini wa kuking’oa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
madarakani kwenye Uchaguz Mkuu ujao, anasema mchakato huo utaishia njiani na ni
kama sehemu ya kuwaongopea Watanzania.
No comments:
Post a Comment