DKT. NNKO AJITOSA KUTIA NIA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KIBAMBA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, June 29, 2025

DKT. NNKO AJITOSA KUTIA NIA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KIBAMBA


NA MWANDISHI WETU


KADA wa   Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt.Walter Nnko, amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania ubunge katika Jimbo la Kibamba.


Dkt Nnko, katika historia yake kwenye siasa kupitia CCM, mwaka 2022 alifanikiwa kushika nafasi ya pili MNEC Mkoa wa Dar es Salaam.


Pia alishika nafasi nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia ngazi ya Kata hadi Wilaya na sasa amechukua fomu ili kutia nia kuwania Jimbo la Kibamba.


Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo leo Juni 29, 2025 ameweka wazi kuwa amechukua jukumu hilo ili kutimiza ndoto yake kupitia siasa.

Leo sina mengi ya kusema kwa maana huu ni mchakato wa kwanza, hivyo hatua nyingine zinaendelea nikifanikiwa jina langu kupita nitaeleza mengi kuhusu dhamira iliyonisukuma kutia nia kuwania ubunge katika jimbo hili la Kibamba" amesema.



"

No comments:

Post a Comment