LEILA MASHA AJITOSA UDIWANI KATA YA KIMARA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, June 29, 2025

LEILA MASHA AJITOSA UDIWANI KATA YA KIMARA


NA MWANDISHI WETU

MWANACHAMA wa Chama  Cha  Mapinduzi (CCM), Leila Masha, kupitia Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania Udiwani Viti Maalumu Kata ya Kimara Jimbo la Ubungo.


Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo, katika Ofisi Kuu Ya Wilaya ya Ubungo, Masha amesema safari ndio imeanza na leo  kuchukua fomu rasmi kutia nia kuwania nafasi hiyo.


"Nadhani kwa sasa sitasema mengi itoshe kusema tayari nimechukua fomu ya kuwania nafasi ya kugombea Udiwani Viti Maalumu Kata ya Kimara na muda wa kampeni ukifika nitasema dhamira iliyonisukuma kuwania nafasi hii," amesema.





No comments:

Post a Comment