TANESCO YATANGAZA KAMPENI YA KUHAMASISHA WATEJA KULIPA MADENI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, June 19, 2025

TANESCO YATANGAZA KAMPENI YA KUHAMASISHA WATEJA KULIPA MADENI

 

NA MWANDISHI WETU

SHIRIKA la Umeme Tanzania(TANESCO) imetangaza kuanza kwa kampeni maalum kwenye maeneo yote nchini ya kuhamasisha ulipaji wa madeni kutoka kwa wateja wa malipo ya baadaya ukaguzu wa mita za LUKU kwa wateja wa malipo kabla.


Kampeni hiyo imepewa jina la "Lipa deni,Linda Miundombinu, Tukuhudumie",ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha ulinzi wa miundombinu ya umeme pamoja na juhudi za kuboresha na kuimarisha uendelevu wa upatikanaji huduma bora ya umeme kwa wananchi.


Taarifa hiyo imetolewa Leo Juni 19,2025 Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa TaNESCO ,Irene Gowelle amesema malengo ya kampeni hii ni kuhamasisha wateja wa malipo ya baada ya kulipa madeni yao kwa hiyari  kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa na kutoa motisha kwa ulipaji wa wakati ikiwemo msamaha wa riba kwa wateja watakaolipa madeni yao kikamilifu.


"Zoezi hili pia litahusisha ukaguzi wa mita za LUKU kwa lengo la kuhakikisha zinafanya kazi vizuri na hazijachezewa na wateja wasio waaminifu, kauli mbiu yake " Huduma endelevu huanza na wewe",amesema


Aidha ,Kaimu Mkurugenzi Gowelle amesema vile vile kuhamasisha umuhimu wa ulinzi shirikishi wa miundombinu ya umeme kwa kuwajumuisha wananchi na kuwapa elimu ya kulinda miundombinu ya Shirika.Miundombinu hii ndio inayowewezesha upatikanaji endelevu wa huduma ya umeme kwa ufanisi hasa kwa kuzingatia kuwa ulinzi wa Miundombinu ya umma ni wajibu kila mwananchi.


Sanjari na hayo pia ameeleza  kwamba Tanesco  inatoa rai kwa  wateja wake wote nchini ambao  wanadaiwa kutoa ushirikiano kwa kulipa madeni yao kwa wakati na hivyo kutoathiri upatikanaji wa  huduma ya umeme kwenye shughulu zao.


Sambamba na hayo Tanesco pia inatoa Rai kwa wananchi kutoa taarifa kuhusu vitendo vya wizi wa umeme au uharibifu na wizi wa  miundombinu ya umeme kwa kushirikiana na vyombo vya dola Ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza kwa ukosefu wa huduma ya umeme pamoja na kuzuia hasara kwa Shirika.

No comments:

Post a Comment