NA MWANDISHI WETU
KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Watu wenye Ulemvu Tanzania (SHIVYAWATA), Jonas Lubago amerejesha fomu za kutia nia kugombea Jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo Julai 2, 2025 baada ya kurejesha fomu katika Ofisi ya Wilaya ya Ubungo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema kama Mtanzania ametumia haki ya Kikatiba kutia nia na kuomba ridhaa kwa chama ya kugombea jimbo hilo.
"Leo nimetimiza haki yangu ya kikatiba kuomba ridhaa ya chama kuomba kuteuliwa kugombea jimbo hili na ikiwa jina langu litarejea nitaeleza kusudia la kugombea," amesema.
Ameongeza kuwa demokrasia ndani ya chama imeongezeka hivyo kupitia nafasi ya makundi maalumu ameona ni vema akaitumia fursa vizuri kutia nia kuwania jimbo hilo.
No comments:
Post a Comment