NA MWANDISHI WETU
KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam Dkt.Walter Nnko, amefanikiwa kurejesha fomu ya kutia nia kuwania ubunge katika Jimbo la Kibamba na kusisitiza kudumisha amani na utulivu katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Dk Nnko amebainisha hayo leo, Juni 2, 2025 baada ya kurejesha fomu hiyo kwenye Ofisi ya CCM Wilaya Jimbo la Ubungo na kuongeza kuwa amani na mshikamano nchi ndio kitu muhimu.
"Leo nimejesha fomu kutia nia ya kuomba ridhaa ya chama kugombea ubunge Jimbo la Kibamba nashukuru mchakato umekwenda vizuri.
"Kikubwa nawasihi watanzania wenzangu kuendelea kudumisha amani ya nchi na nashukuru mchakato wa kuchukua na kurejesha umekwenda vizuri kwani tumepokelewa vizuri na viongozi wa Wilaya na sasa tunasubiri mchakato ndani ya chama kwa ngazi zote.
"Majina matatu ndio yatakayorudi kuingia kwenye kinyang'anyilo cha kumpata mgombea ubunge wa jimbo hili, yeyote atakayepita tutamshika mkono kuhakikisha CCM inapata ushindi mkubwa Oktoba mwaka huu, amesema.
No comments:
Post a Comment