YAMUNGU AREJESHA FOMU YA KUTIA NIA KUGOMBEA JIMBO LA KIBAMBA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, July 1, 2025

YAMUNGU AREJESHA FOMU YA KUTIA NIA KUGOMBEA JIMBO LA KIBAMBA


NA MWANDISHI WETU


KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nestory Yamungu amefanikiwa kurejesha fomu za kuomba ridhaa ya kugombea ubunge katika Jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam.


Yamungu, baada ya kurejesha fomu hizo leo Julai 1, 2025 katika Ofisi za CCM Wilaya ya Ubungo, amefafanua kwamba anashukuru kutumia haki yake ya kikatiba katika hatua hiyo ya kwanza ya kuomba ridhaa kwa wajumbe kuwa mgombea wa jimbo hilo.


"Nashukuru mambo yamekwenda vema na nimefanikiwa kujaza fomu na kuzirejesha, hivyo nasubiri hatua inayofuata ya mchujo kupitia wajumbe na ngazi nyingine," anasema.


Anafafanua kuwa ikiwa atafanikiwa kupenya katika hatua zilizosalia na kupata ridhaa ya kugombea  ataeleza sera zake na makusudio yake ikiwa atakuwa mbunge nini atafanya katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Jimbo la Kibamba.

No comments:

Post a Comment