USHIRIKI WA TAWA KATIKA MAONESHO YA 49 YA BIASHARA YA KIMATAIFA UNAVUTIA WANANCHI WENGI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, July 1, 2025

USHIRIKI WA TAWA KATIKA MAONESHO YA 49 YA BIASHARA YA KIMATAIFA UNAVUTIA WANANCHI WENGI

 


NA MWANDISHI WETU


MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) inashiriki katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa kwa mwaka 2025 yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere, vilivyopo barabara ya Kilwa, Jijini Dar es Salaam.


 Kupitia maonesho hayo, TAWA inatumia fursa hiyo kutangaza bidhaa na huduma mbalimbali zinazohusiana na utalii na uhifadhi zinazotolewa na Mamlaka hiyo.


Aidha unapotembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii, utakutana na maofisa wa TAWA ambao watakupa maelezo kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo fursa za Uwekezaji zinazopatikana katika maeneo mbalimbali yaliyo chini ya usimamizi wa TAWA, ikiwa ni pamoja na Makuyuni Wildlife Park (Arusha)

Nyingine ni Pande (Dar es Salaam),Wami-Mbiki (Morogoro na Pwani),Tabora Zoo (Tabora),Ruhila Zoo (Ruvuma) na mengine mengi


Pia utapata fursa ya kujionea Wanyamapori Hai kupitia bustani ya wanyamapori iliyopo ndani ya banda la Wizara ya Maliasili na Utalii, kwa viingilio vya bei nafuu kwa Watanzania.

Aidha utaona  vivutio vya Utalii vilivyopo katika maeneo mbalimbali yanayosimamiwa na TAWA, pamoja na taarifa za gharama na namna ya kuyatembelea.


Pamoja na hayo kuna ofa maalum ya ziara ya kutembelea Hifadhi ya Pande, iliyopo Jijini Dar es Salaam, kwa gharama nafuu katika msimu huu wa Maonesho ya Sabasaba.


Utaelezwa  shughuli za Utalii na Uhifadhi zinazofanywa na TAWA, ikiwa ni pamoja na elimu kwa umma kuhusu namna ya kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu, na kuelewa tabia zao.


Katika maonesho hayo kuna  Nyamapori Choma iliyoandaliwa kwa umahiri na kwa kuzingatia ubora wa hali ya juu Kwa bei ya kizalendo.


Hivyo wananchi wote wanakaribishwa kwa wingi katika banda la Wizara ya Maliasili na Utalii, kujifunze, kuelimishwa na kujionea huduma na vivutio vya kipekee, hasa wanyamapori hai waliopo ndani ya banda hilo.





No comments:

Post a Comment