NA MUSA JUMA, IDDIS ABABA
WAANDISHI wa Habari Afrika watakiwa kukuza Kilimo ikolojia kwa usalama wa chakula Afrika.
Wito huo kwa wanahabari umetokana na kuwepo kwa ongezeko la uzalishaji na usambazaji wa vyakula ambavyo vimetokana na kilimo cha kemikali za viwandani na kupuuzwa kwa vyakula vinavyopatikana kwa mbegu za asili ya Afrika.
Hali hii inatoka na mtizamo hasi kuwa Kilimo Ikolojia kuwa hakina tija na ni cha kujikimu tu na hakiwezi kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya chakula jambo ambalo linapaswa kuelezwa kwa ukweli hasa ikizimgatiwa kumekuwepo na athari za kiafya na kimazingira kutokana na matumizi ya mbegu,mbolea na viuatilifu vya viwandani.
Akifungua mafunzo hayo kwa wanahabari Afrika kuhusiana na Ujasiriamali wa Kilimo-Ikolojia Afrika na Masoko kwa ajili ya Uhuru wa Chakula Afrika yaliyoandaliwa Shirika la Alliance for Food Sovereignty in Africa (AFSA) Mratibu wa miradi wa shirika hilo, Bridget Mugambe alisema ni muhimu sana wanahabari barani Afrika kusaidia kuandika vizuri umuhimu wa kilimo Ikolojia Afrika.
Alisema kumekuwepo na habari za kupotoshwa zisizo na ushahidi wa wazi juu ya mifumo ya kilimo Ikolojia ambacho, mizizi yake imejikita katika maarifa ya asili na uwezo wake wa kuleta manufaa ya kiafya, kiuchumi na kiikolojia.
"Mchango wa kilimo Ikolojia barani Afrika unaelezwa kuwa ni ndogo haustawi na hauchangii kikamilifu uchumi wa kisasa jambo ambalo sio kweli"alisema
Afisa mradi wa Masoko na Ujasiriamali wa AFSA Ruth Nabaggala alisema wanahabari wanapaswa kupinga upotoshaji juu ya kilimo lkolojia na masoko yake kwa kuandika habari sahihi na zinazoinua hadhi ya uhuru wa chakula Afrika.
Alisema kuna ushahidi kutoka nchi za Ghana, Tunisia, na Zimbabwe unaonesha kuwa biashara za kilimo-Ikolojia zinakidhi mahitaji halisi. Matunda na mboga ndizo bidhaa zinazotafutwa zaidi, zikifuatiwa na nafaka.
"Wateja wako tayari kuunga mkono mifumo hii kwa 62% ya waliojibu utafiti walionesha utayari wa kulipa zaidi kwa bidhaa za kilimo-Ikolojia, na 53% wako tayari hata kufadhili wakulima kabla ya mavuno"alisema
Hata hivyo alisema licha ya kuwepo na upotoshwaji bado pia hakuna sheria na sera rafiki za kuendeleza kilimo Ikolojia kwa nchi nyingi barani Afrika.
Akiwasilisha mada kuhusiana na nafasi ya Ujasiriamali wa Kilimo Hai(Ikolojia) na Masoko katika kuleta Mageuzi ya Mfumo wa Chakula Afrika Dr Mamadou Goita.....alisema soko la mazao ya chakula limedhibitiwa na makampuni makubwa kutoka nje ya Afrika.
Alisema makampuni hayo ndio ambayo.yanasambaza mbegu,mbolea na viatilifu na hivyo kudidimiza ukuwaji wa kilimo Ikolojia licha ya umuhimu wake mkubwa kwa usalama wa chakula.
"Kama bara la Afrika linataka kuwa na usalama wa chakula lazima litahakikishe linauwezo wa kuzalisha na kusambaza mbegu na mazao yake ya asili ambayo kimsingi ni bora kuliko kutegemea kampuni za nje"alisema
Alisema mustakabali wa chakula Afrika unatakiwa kujikita katika kilimo endelevu cha kiikolojia kinacholinda haki za kijamii, kukuza ajira, kulinda bayoanuwai, na kuboresha afya ya udongo na mazingira.
Waandishi wa habari Waandamizi kutoka nchi kadhaa Afrika ikiwepo, Tanzania,Kenya,Uganda,Malawi,Zambia,Togo,Tunisia,Zimbabwe,Ghana,Burkinafaso na wenyeji ,Ethiopia wanashiriki mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment