WABUNGE WALIOPITA VUNJO NI DARASA TOSHA KWANGU: LYIMO - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, July 24, 2025

WABUNGE WALIOPITA VUNJO NI DARASA TOSHA KWANGU: LYIMO


Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) Richard Lyimo. (
Picha Kwa hisani ya mtandao)


NA MWANDISHI WETU

MWENYEKITI wa Tanzania Labour Party (TLP) Richard Lyimo, ambaye ni mtia nia katika Jimbo la Vunjo, mkoani Kilimanjaro, amesema ikiwa atapata ridhaa ya chama chake kuwania ubunge atumia madhaifu ya wabunge ambao wamepita kuomba kura kwa wananchi.

Kwa mujibu wa Lyimo, anayajua madhaifu mengi ya wabunge waliopita katika jimbo hilo hali iliyosababisha kushindwa kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitamani kuwa nayo na kuyashuhudia yakifanyika katika majimbo mengine.

“Nikipata ridhaa ya chama changu kuwania ubunge Vunjo nitaingia katika kinyang’anyilo cha uchaguzi kama mchezaji wa akiba, kwani nimeshashiriki chaguzi nyingi na nimeona wapi wanakosea na kwa nini wanashindwa kuwaletea wananchi maendeleo.

“Hivyo kwa wabunge ambao wamepita kwangu walikuwa ni darasa tosha itakayonifanya kufanya kazi yangu kwa ufanisi mkubwa ikiwa nitachaguliwa kuwa Mbunge wa Vunjo kwa maana nimeshajua wapi waliotangulia walikuwa wanakosea na kushindwa kuwaletea wananchi maendeleo,” amesema.

 Amesema kazi ya siasa sio ya kutoka darasani eti kwa kuwa una PHD au unatoka ofisini moja kwa moja na kugombea ukadhani unaweza kuwaletea maendeleo wananchi la hasha, siasa inahitaji uzoefu ambao amejinasibu anao na atahakikisha anautumia kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi.

“Muda wa kampeni ukifika, nitasema mengi na wananchi wa Vunjo watanielewa kwa maana nitawaeleza ukweli wapi waliotangulia walishindwa katika kuwaletea maendeleo na njia nitakazotumia kulifanya jimbo hilo kuwa na maendeleo, ikiwemo kutumia vizuri Mfuko wa Jimbo,” amesema

No comments:

Post a Comment