KADA wa ACT wazalendo Monalisa Ndala, ambaye amevuliwa uanachama amekitaka chama hicho kujitafakari na kupinga 'kuvufungashiwa virago' akibainisha yeye bado ni mwanachana halali kutokea Dar es Salaam na si Iringa.
Amefafanua kuwa alichokifanya ni kuonesha chama wapi kuna tatizo na si kushindwa kutekeleza katiba ya chama kama ilivyoeleza taarifa zilizotolewa na uongozi wa Chama hicho kwa madai ya kushindwa kutekeleza katiba ya Chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari leo 30,agosti 2025 Sinza,jijini Dar es salaam Monalisa amesema kuwa yeye Bado ni mwanachama wa ACT aliyesajiliwa Dar es salaam na sio Mafifi mkoani Iringa .
"Nimempa Katibu Mkuu siku mbili anapaswa atoke hadharani aikanushe ile barua kwa sababu Mimi ni mwanachama,mwenezi wa mkoa wa Dar es salaam pia ni Mwenyekiti wa Jimbo la kibamba nawezaje kuwa mwananchi wa kata ya Mafifi".
"Mambo haya hayatasaidia Chama zaidi ya kuishangaza jamii kwa hiyo Katibu Mkuu inabidi anusuru na anapaswa aseme barua sio rasmi na baada ya juma hili nitafuata hatua sahihi na tusilaumiane".ameeleza Monalisa.
No comments:
Post a Comment