DKT MAKALA: UELEWA WA TIBA MBADALA UMEONGEZEKA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, August 20, 2025

DKT MAKALA: UELEWA WA TIBA MBADALA UMEONGEZEKA


NA MWANDISHI WETU, DOHA

Mkurugenzi Mtendaji na Daktari wa kampuni ya Norland Global Tanzania, Dkt Moses Makalla amesema uelewa wa watu wengi juu ya umuhimu wa tiba asili/mbadala umechangia ufanisi wa ukuaji wa sekta ya afya Tanzania.


Akizungumza na waandishi wa habari nchini Qatar ambako yupo kwa ajili ya kutoa mafunzo na kutibu wananchi wenye changamoto mbalimbali za kiafya, Dkt Makalla ambaye kampuni yake inajihusisha na utafiti, uzalishaji na usambazaji wa bidhaa za tiba mbadala amesema mafanikio makubwa yamepatikana kutoka kwa watumiaji wa sehemu mbalimbali kwa kutibu chanzo cha tatizo ikiwemo magonjwa yasiyoambukiza.


“Bidhaa zetu zinatengenezwa nchini China ambako ni makao makuu ya kampuni hii, bidhaa hizi zimekuwa na msaada mkubwa na kutegemewa kuanzia nchini China mpaka katika bara la Afrika hususani kwa nchi za Afrika Mashariki kwa wagonjwa na watumiaji wake “, alisema Dkt Makalla.


Kwa mujibu wa Dkt Makalla aliweka wazi kuwa licha ya Norland Global Tanzania yenye ofisi zake katika jiji la Arusha, Dar es Salaam na Doha nchini Qatar, pia wana mipango ya kufungua ofisi nyingine katika majiji ya Dodoma, Mwanza na Mbeya kwa kuanzia.


Dkt Makalla alisema wamekuwa wakipokea wagonjwa na watumiaji wa bidhaa hizo kutoka katika mikoa mbalimbali, hivyo wameona kuna kila sababu ya kuwasogezea huduma katika mikoa ya karibu nao.


“Ninafarijika kusema kuwa Watanzania wameanza kuelewa shughuli zetu kwani tunatoa vipimo kabla ya kuhudumia mgonjwa ili tuweze kubaini tatizo alilo nalo na kumpatia tiba sahihi”, alisema na kuongeza kuwa afya ni kitu muhimu sana katika maisha ya binadamu. 


Mbali na kufurahishwa na mrejesho kutoka kwa wagonjwa na watumiaji wa tiba na dawa hizo za asili, Dkt Makalla amewashauri Watanzania kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara kwani maradhi mengine hayana dalili za moja kwa moja, ila kwa kupima afya huweza kubainika.


“Napenda kupongeza juhudi zinazowekwa na Serikali, kwa kutengeneza miundombinu imara ya kuimarisha sekta ya afya kwa mijini nna vijijini”, alisema Dkt Makalla.


Dkt Makalla yupo nchini Qatar akiendelea kutoa matibabu sambamba na mafunzo kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za asili kutoka Norland. 




No comments:

Post a Comment