MWANDISHI WETU
MTIA nia wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo, leo anatarajia kuchukua fomu rasmi ya kuomba kuteuliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), katika Ofisi za Makao Makuu ya Tume hiyo Dodoma.
Chama cha NLD kinawaalika waandishi wote wa habari nchini pamoja na wananchi wote wenye mapenzi mema na demokrasia kumsindikiza Doyo Hassan Doyo katika hatua hii muhimu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Karibuni tushuhudie tukio hili la kihistoria katika safari ya mabadiliko ya kweli kwa Taifa letu.





No comments:
Post a Comment