NA MWANDISHI WETU
MKUTANO Mkuu Maalum wa chama umeidhinisha Gombo Samandito kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku Eng. Hamad Masoud Hamad akichaguliwa kuwa mgombea urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Uchaguzi huo ulifanyika kufuatia mchuano mkali kati ya watia nia watano, ambapo wajumbe wa mkutano mkuu walipiga kura kuwapata washindi.
Aidha, mkutano huo ulipitisha kwa kauli moja uteuzi wa Katibu Mkuu wa chama, Mhe. Husna Mohammed Abdalla, kuwa mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano, baada ya kupendekezwa na Mhe. Gombo Samandito Gombo.
Kwa upande wa Tanzania Bara, miongoni mwa watia nia alikuwa Mhe. Nkunyuntila Siwale. Nchini Zanzibar, Eng. Hamad Masoud Hamad aliwania nafasi hiyo akipambana na Mhe. Eng. Habib Mnyaa na Mhe. Dkt. Mohamed Mikidadi.
Mkutano Mkuu Maalum huo, uliofanyika Agosti 9, 2025 katika Ukumbi wa Lekham, pia uliidhinisha ilani za uchaguzi kwa uchaguzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ule wa Zanzibar







No comments:
Post a Comment