MBETO: RAIS DKT. SAMIA 'CHAMPION' WA KUSAKA TURUFU ZA KISIASA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, August 24, 2025

MBETO: RAIS DKT. SAMIA 'CHAMPION' WA KUSAKA TURUFU ZA KISIASA


NA MWANDISHI WETU, DODOMA

CHAMA Cha Mapinduzi  (CCM)kimesifu  uwezo mkubwa  wa kisiasa alionao Mwenyekiti  wa CCM , Rais Dk Samia Suluhu  Hassan katika mkakati wa  kusaka turufu za kisiasa kuelekea ushindi wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba Mwaka huu.


Pia CCM kimejigamba kuwa kina hazina kubwa ya Wanasiasa wenye Uwezo, Vipaji ,Ufahamu na Uzoefu  katika medani za Uongozi , Diplomasia  na  Siasa.


Katibu  wa Kamati  Maalum  ya NEC  Zanzibar , Idara ya Itikadi, Uenezi  na Mafunzo , Khamis  Mbeto Khamis, ameeleza hayo  kufuatia uteuzi wa Katibu  Mkuu  mpya wa CCM , Dk Asha-Rose Migiro na  kufanyika kwa mabadiliko madogo katika safu ya sekreteriat ya NEC .


Dk Migiro amechukua nafasi ya  aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM,  Balozi  Mstaafu  Dk  Emmanuel Nchimbi ambaye  ameteuliwa kuwa Mgombea Mwenza wa Urais  CCM. 


Mbeto  alisema CCM ni chama kikubwa kinachojitegemea mtaji wa   nguvu na idadi ya  wanachama wake, viongozi walioshiba uzalendo , uzoefu ,upeo na  amana katika jamii .


Akitaja kuteuliwa kwa Dk Migiro kuwa Katibu  Mkuu mpya wa CCM, alisema  ni kama  kimbunga  Hidaya kuelekea  kukipatia   ushindi  chama hicho   ifikapo Oktoba Mwaka huu .


"Rais Dk Samia ni bingwa  wa kusoma alama za nyakati katika kusaka piku na turufu za  ushindi . Chama chetu kina hazina    ya viongozi isiofilisika. Hakisubiri  kuzoazoa mabaki yanayosazwa  na wengine " Alisema Mbeto 


Aidha , Katibu huyo Mwenezi , alisema uteuzi wa Dk Migiro kuwa Katibu  Mkuu CCM  ni   ufunguo mpya  utakaofungua kufuli  za milango yote  yenye  kutu hatimaye  kukipatia ushindi CCM usio na  longolongo .


'Kwa wale wote wanaotaka  kuitikisa CCM watakumbana na nguvu zake za asili  .Nguvu za CCM ni zaidi  ya Tufani, Kimbunga na Tsumani. Tungependa wajue siku  zote  kina cha maji  hakipimwi kwa kutumia kijiti au kutazama kwa macho" Alieleza . 


Akifafanua zaidi, Mbeto alisema kelele zinazopigwa na baadhi ya  mamluki wa ksiasa wasiolitakia mema Taifa letu  zinasikika, lakini  akasema majibu  ya watu  hao ,yatajibiwa kutokana na matokeo ya Uchaguzi  Mkuu .


"Nguvu na mtaji wa ushindi wa  CCM  hutokana na ridhaa ya watu.  Kwa miaka yote CCM kimeshughulika na utatuzi wa  changamoto za maendeleo ya watu. Watu wanakiheshimu  , wanakitegemea na  kukiamini "Alisisitiza Mbeto

No comments:

Post a Comment