CCM PWANI CHAWAITA WANANCHI KUMLAKI DK SAMIA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, September 27, 2025

CCM PWANI CHAWAITA WANANCHI KUMLAKI DK SAMIA


NA MWANDISHI WETU, KIBAHA


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani kimewaita wakazi wa Mkoa huo kujitokeza kwa wingi kumlaki mgombea wake wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kesho Septemba 28 mwaka huu.


Akizingumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake mjini Kibaha Katibu siasa uenezi na mafunzo CCM Mkoa wa Pwani David Mramba amesema kuwa mgombea huyo atafanya mkutano kwenye viwanja Saaba Saba Kata ya Mkuza Wilaya ya Kibaha.


Mramba amesema kuwa mbali ya kufanya mkutano huo mkubwa wa kampeni pia atafanya mikutano midogo huko Chalinze na Msata Wilaya ya Bagamoyo.


"Lengo la mkutano huo ni kuwasilisha ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2025/20230, kuonyesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kwenye awamu ya sita na kuwashukuru wananchi kwa kuendelea kuikiamini Chama Cha Mapinduzi,"amesema Mramba.


Amewaomba wananchi wa Mkoa huo kujitokeza kwa wingi kuhudhuria mkutano huo ili kwenda kumsikiliza mgombea wa CCM ili Oktoba 29 mwaka huu wakajitokeze kumpigia kura za kishindo ili aendelee kuiongoza nchi.


No comments:

Post a Comment