CHUO CHA FURAHIKA ISLAMIC VOCATIONAL CHATANGAZA KUSOMESHA BURE WAHITIMU DARASA LA SABA, KIDATO CHA NNE - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, September 26, 2025

CHUO CHA FURAHIKA ISLAMIC VOCATIONAL CHATANGAZA KUSOMESHA BURE WAHITIMU DARASA LA SABA, KIDATO CHA NNE


NA MWANDISHI WETU

WAKAZI wa Zanzibar wametakiwa kujitokeza kwa wingi kusoma bure masomo ya Ufundi na Hoteli katika Chuo cha Furahika Islamic Vocatinal Centre chenye usajili namba VTC/PRP/2025/0001/01 ikiwa ni moja ya tawi la Chuo cha Furahika Dar es Salaam.

Dkt. David Msuya ambaye ni Mkuu wa Chuo Cha Ufundi Furahika jijini Dar es Salaam ametoa wito huo leo, Septemba 26, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kubainisha kwamba masomo katika chuo hicho ambacho kipo Kituo cha Darajani Zanzibar yataanza Oktoba 20, 2025 na udahili wa wanafunzi ukitaraji kuanza wiki ijayo.

 “Tumefungua Chuo Cha Ufundi pale Kituo Cha Darajani ghorofa ya pili na kozi zitazofundishwa kwa wanafunzi wa dini zote ni Makeup, Information Communication and Technology (ICT), English Language, French, Secretarial, Tourism, Event Planning Management, Food and Baverage Services zitafundishwa bure kwa vijana wote waliomaliza kidato cha nne na darasa la saba na kushindwa kuendelea na masomo kwa sababu mbalimbali,” amesema.

Ameongeza kuwa lengo la kutoa elimu bure ni kuunga mkono Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inayoongozwa na Rais Dkt Hussein Alli Mwinyi katika jitihada zake za kuwakwamua na kuwaendeleza vijana  katika elimu ya kujitegemea ili waondokane na utegemezi.

Dkt Msuya alifafanua kuwa awali wanafunzi hao kutoka Zanzibar walikuwa wanakwenda katika Chuo Cha Furahika Dar es Salaam kusoma fani mbalimbali na mwaka jana wanafunzi 400 walihitimu mafunzo katika kazi ikiwemo Hoteli, umeme wa magari, Makeup, ufundi nguo na nyinginezo.

Amesema kutoka na kuwepo kwa gharama kubwa za malazi na chakula kwa wanafunzi hao, ndipo wakaamua kufungua chuo Zanzibar ili kupunguza hadha na sasa wahitaji wanaweza kujiunga na chuo kilichopo Darajani.

 

Kutokana na kuwasogezea huduma hiyo kariu tunawaomba wazazi wawalete watoto wao hapo ili wapate elimu bure itakayowafaa katika maisha yao na kuwaondoa katika hatari ya kujiunga katika makundo ovu ya uasherati.

No comments:

Post a Comment