KATAENI KUCHAGULIWA VIONGOZI NA WATU WENGINE – MANG'ATI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, September 28, 2025

KATAENI KUCHAGULIWA VIONGOZI NA WATU WENGINE – MANG'ATI



NA MWANDISHI WETU

MGOMBEA Udiwani wa Kata ya Pugu jijini Dar es Salaam, kupitia Chama Cha Mapinduzi  (CCM), Frank Mang'ati, amewataka wananchi wa kata hiyo kukataa kuchaguliwa viongozi na watu wengine kwa maana kura zao ndio sauti zao, hivyo wajitokeze kwa wingi Oktoba 29, 2025 kupigia kura CCM

Mang'ati amesema hayo, Septemba 24, mwaka huu  jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii na kufafanua kuwa ikiwa atachaguliwa kuwa diwani wa kata hiyo atashirikiana na wananchi kutekeleza vipambele vyake kwa umahili mkubwa ambavyo ameviahidi.

Amesema baadhi ya vipaumbele hivyo ni pamoja na ujenzi ya Kituo cha Afya katika eneo la  Kinyamwezi ambako kuna eneo la wazi lisilohitajika kulipa fidia ya aina yoyote na kinachohitajika ni usimamizi wa kukamilisha mchakato huo, pia ujenzi wa uzio katika Zahanati ya Pugu.

Pia ameongeza kuwa jambo lingine ambalo atakwenda kulifanya ikiwa atakuwa diwani wa kata hiyo ni kuhakikisha barabara zote za mitaa ambacho zimekuwa korofi kwa  kipindi kirefu husuan wakati wa mvua zitajengwa kwa kiwango bora na kuwekewa makaravati ili kupitisha maji kwa usahihi bila kuharibu miundombinu.

Tofauti na hayo, Mang'ati amesema katika uongozi wake atahakikisha kwa kushirikiana na wananchi unajengwa uzio katika Shule ya Sekondari Kinyamwezi ili kuiweka katika mazingira mazuri kwa wanafunzi na kusaidia kuongeza utukivu.

Pia amesema atambua kazi kubwa ambayo imefanywa na uongozi uliopita hususan kwemye ujenzi wa shule ikiwemo za Msingi na Sekondari katika uongozi wake atahakiksha anaongeza madawati katika shule hizo na kujenga shule nyingine ya msingi katika Mtaa wa Mustapha ili kwapunguzia kutembea umbali mrefu wanafunzi wa eneo hilo.

Aidha ameongeza kuwa katika baadhi ya maeneo ya Kimani kukosa umeme, ikiwa ataingia madarakani atakahakikisha yanapata umeme ili kuinua maisha ya wananchi kupata nishati hiyo muhimu kwa maendeleo ya mtaa na taifa kwa ujuma.

“Wito wangu kwa kila mwananchi mwenye sifa ya kupiga kura, Oktiba 29, si siku ya siasa ni siku ya kwenda kufanya maamuzi kwa ajili ya hatma ya maisha yetu, tusikubali mtu atuchagulie hatma ya maisha yetu hatima ya maisha yetu ipo katika mikono yetu kwenda kutia tiki kwa Dkt Samia Suluhu Hassan, kutia tiki kwa mbunge Jerry Silaa na kutia tiki kwangu Frank Mang'ati niwe diwani wa kata hii, Sisi ndio tuna uwezo wa kwenda kutatua kero za wananchi.

No comments:

Post a Comment