MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha NLD, Doyo Hassan Doyo, akiwa katika ziara za kampeni Wilaya ya Serengeti, aliwahutubia wakazi wa Mji wa Mugumu.
Katika hotuba yake, Doyo alisema kuwa ni fedheha kwa wananchi wa Serengeti kukosa miundombinu bora ya barabara, hususan barabara za kiunganishi.
Alitolea mfano wa baadhi ya mikoa ya Kaskazini ambayo tayari imeunganishwa vizuri kwa barabara na miundombinu mingine ya usafiri, hali ambayo imeboresha maisha ya wananchi na kurahisisha biashara katika maeneo ya vijijini.
Aidha, Doyo ameahidi kwamba, endapo wananchi wa Serengeti watamchagua yeye pamoja na serikali yake, watahakikisha wanajenga barabara za kiwango cha juu, ikiwemo barabara ya Zege, sambamba na miundombinu yote muhimu inayohitajika ili kuhakikisha Wilaya ya Serengeti inakuwa na kiunganishi cha kisasa, chenye ubora na tija kwa wananchi.
Mhe. Doyo alisema. “Nitaunganisha Serengeti na Bunda, Arusha na maeneo mengine, ili mji huu uwe na tija kijamii na kukuza uchumi endelevu kwa vizazi vyenu. Ilani ya NLD imewaangalia kwa makini wananchi wa Mkoa wa Mara na Tanzania kwa ujumla.”
Msafara wa mgombea urais huyo wa NLD, sasa upo mkoani Mara kuanza rasmi ziara ya kampeni katika Mikoa ya kanda ya Ziwa.
No comments:
Post a Comment