MAENEO 12 YAAZIMIWA KUFANIKISHA DIRA YA MAENDELEO 205O - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, October 10, 2025

MAENEO 12 YAAZIMIWA KUFANIKISHA DIRA YA MAENDELEO 205O


NA MWANDISHI WETU


WASHIRIKI wa Kongamano la nafasi ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), lilofanyika Chuo Kikuu cha Ruaha  (RUCU) limeazimia maeneo 12 ambayo yatafanikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.


Maazimio hayo yamefikiwa baada ya mjadala ulioshirikisha wanataaluma kutoka maeneo mbalimbali ambapo walikubaliana kuwa azimio la kwanza ni kuhakikisha ubia kati ya sekta ya umma na binafsi unakuwa na nafasi muhimu katika kuchochea maendeleo ya nchi na kufikia malengo ya Dira 2050.


Azimio la pili ni ubia kati ya sekta ya umma na binafsi kuipunguzia mzigo serikali ili ijikite zaidi katika maeneo ya huduma za jamii ambazo hazivutii sekta binafsi.


"Ubia kati ya sekta ya umma na binafsi sio uuzaji au ubinafsishaji bali ni mashikirikiano ya pamoja ambayo yanaweza kufikia tamati pale inapobidi;


Ubia unaiondolea serikali shinikizo la kukopa ili kutekeleza miradi mbalimbali badala yake sekta binafsi inashiriki kufadhili miradi muhimu kupitia ubia,"amesema.


Washiriki hao waliazimia kuwa yapo maeneo mengi hadi ngazi za halimashauri ambayo badala ya serikali kuwekeza moja kwa moja sekta binafsi inaweza ikafanya kwa ushirikiano na serikali. Mfano ujenzi wa maegesho au masoko.


Eneo lingine ni elimu kuwa nyenzo muhimu katika kufanikisha Dira 2050

mabadiliko ya mtaala wa elimu kutoka ule unaoegemea katika maarifa hadi ule wa umahiri, ni nyenzo mwafaka katika kufikia malengo ya Dira 2050.


Pia wamesisitiza  uwekezaji mkubwa katika kuwajengea uwezo walimu watekeleze kwa ufanisi mtaala mpya.


Azimio la nane ni elimu inayotolewa lazima iweke pia mkazo mkubwa  kufanikishaau kujenga maadili na thamani miongoni mwa wanafunzi ili kufikia vema malengo ya Dira 2050.


"Tisa kuna haja ya kuboresha zaidi mkakati wa mawasiliano ili miradi ya PPP sio tu iweze kueleweka vema kwa watu wote bali iwe jumuishi kwa makundi yote ili kufikia kwa vitendo malengo ya Dira 2050


Dira 2050 inamatumaini ya kushughulikia changamoto za vijana ikiwa ni pamoja na suala la ajira, kuzingatia utawala wa sheria, umoja wa kitaifa, ushirikishaji, kupambana na rushwa, na kushirikisha serikali za mtaa na uchumi jumuishi sio tu ni ule unaowasaidia wengi bali pia unatoa fursa kwa wengi kushiriki katika uchumi,"walisisitiza.

No comments:

Post a Comment