OSHA YAWAELIMISHA WATU WASIOONA KUHUSU AFYA NA USALAMA KAZINI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, October 6, 2025

OSHA YAWAELIMISHA WATU WASIOONA KUHUSU AFYA NA USALAMA KAZINI


NA MWANDISHI WETU,PWANI

WAKALA wa Usalama na Afya Mahala paKazi (OSHA), imetoa elimu watu wasioona wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kwa lengo la kuwawezesha kushiriki shughuli za uzalishaji mali kwa kuzingatia kanuni bora za Usalama na Afya kazini.


Mafunzo hayo ya siku moja ambayo yametolewa kwa wanachama 50 wa jumuiya ya wasioona Tanzania ( TAB) yamehusisha mada mbalimbali zikiwemo utambuzi na udhibiti wa vihatarishi vya Usalama na Afya pamoja na misingi ya huduma ya kwanza Mahali pakazi.


Washiriki wa Mafunzo hayo wanajihusisha na shughuli mbalimbali zikiwemo Ushonaji, kilimo, ufugaji, uzalishaji wa bidhaa zikiwemo sabuni na biashara ndogo ndogo.


Akifungua Mafunzo hayo Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, amesema Taasisi anayoiongoza inatambua thamani na mchango wa watu wenye Ulemavu katika kujenga uchumi wa Taifa jambo ambalo limepelekea Mafunzo hayo kuandaliwa pamoja na Mafunzo mengine ambayo (OSHA) imekuwa ikiyatoa kwa makundi mbalimbali ya watu wenye Ulemavu.



"Niwapongeze washiriki wote wa Mafunzo kwa kuitikia mwaliko wa kushiriki Mafunzo haya muhimu kuweza kwanini dhahiri kuwa Ulemavu ni hali tu ambayo hazipaswi kuwa kikwazo kwenu kushiriki katika shughuli za kiuchumi" amesema Mtendaji Mkuu wa OSHA na kuongeza;


" Sambamba na Mafunzo haya, tunawapatia vifaa saidizi zikiwemo fimbo nyeupe, karatasi za nukta nundu pamoja na vitabu maalumu vya nukta nundu vyenye maudhui ya Mafunzo ya usalama na Afya kwa ajili ya rejea zaidi."


Aidha Mwenda ameahidi kuwa Mafunzo ya usalama na Afya kwa makundi mbalimbali ya watu wenye Ulemavu yatafuatiwa na zoezi la kutembelea maeneo yao ya kazi kwa ajili ya kutathmini mazingira ya kazi Ili kushauri namna sahihi ya kuboresha mazingira hayo


Awali akiwasilisha salamu za jumuiya ya wasioona Tanzania mwenyekiti wa jumuiya hiyo Omary Itambu, ameipongeza OSHA kwa kuwa mstari wa mbele katika kuwawezesha watu wasioona pamoja na Makundi mengine ya watu wenye Ulemavu.



"Tunaiomba OSHA kuendeleza utamaduni huu wa kutujali watu wenye Ulemavu. Kwa niaba ya washiriki wenzangu niwahakikishie OSHA kuwa Mafunzo waliotupatia si tu yatakwenda kuimarisha afya na Usalama wetu bali yatatusaidia sana kuongeza thamani ya huduma wa bidhaa tunazozalisha," amesema Itambu.


Aidha Itambu ametoa wito kwa washiriki wenzake wa Mafunzo kuwa mabalozi waziri wa OSHA ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wenzao ambao hawakupata fursa ya kushiriki Mafunzo.


Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki wengine wa Mafunzo, mratibu wa idara ya vijana wa jumuiya ya wasioona Bakari Hassani amesema jambo lililofanywa na OSHA ni la kuigwa na Taasisi zingine za kiserikali na zisizo za kiserikali. Akisisitiza kwamba Mafunzo hayo na vifaa saidizi walivyopewa vitarahisisha utendaji na kuongeza tija katika shughuli zao za kila siku.

No comments:

Post a Comment