MPOGOLO AWATAKA POLISI KUWAKAMATA WALIOMUUA MZEE SALEHE - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, December 28, 2025

MPOGOLO AWATAKA POLISI KUWAKAMATA WALIOMUUA MZEE SALEHE

Mkuu wa wa Wilaya ya Ilala , Edward Mpogolo akizungumza na wanananchi wa Mtaa wa Zavala Kata ya Buyuni wilaya ya Ilala Dar es Salaam kufuatia mauaji ya Mzee Salehe Idd Salehe yaliyofanyika Desemba 4, 2025.
............................................................

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

MKUU wa Wilaya ya Ilala , Edward Mpogolo ameliagiza Jeshi la Polisi kupitia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, ACP Yustino Mgonja kutumia utaalamu na timu yake kuwakamata mara moja kundi la watu waliofanya mauaji ya mwananchi Salehe Idd Salehe.
-
Salehe ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Zavala Kata ya Buyuni wilaya ya Ilala Dar es Salaam alivamiwa akiwa nyumbani kwake na watu wasiyojulikana Desemba 4,2025 majira ya saa 11:00 alfajiri na kufariki njiani wakati akipelekwa Hospitali ya Amana kupatiwa matibabu.
-
Mpogolo alitoa agizo hilo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Zavala mara baada kupata taarifa za mauaji hayo ya kinyama dhidi ya mzee huyo.
-
Akizungumza katika mkutano huo, Mpogolo alisema Mzee Salehe katika maisha yake alikuwa mzalendo wa kweli kwa kupigania maeneo ya wazi ya Serikali mfano shule, masoko na vituo vya afya yasichukuliwe na genge la wahalifu wanaouza maeneo hayo.

Maeneo yaliyokuwa yakivamiwa ni ya wazi na viwanja ambavyo tayari vilikuwa vimepimwa na Serikali katika Programu ya viwanja elfu 20 Kata ya Buyuni kati ya miaka ya 2003/2005.
Mkuu wa wa Wilaya ya Ilala , Edward Mpogolo, akiwa na viongozi mbalimbali katika kata hiyo wakati alipokwenda kuzungumza na wananchi.
Wananchi na viongozi wakielezea kuhusu tukio hilo.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.

 

No comments:

Post a Comment