NA MWANDISHI WETU
MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekamata kilogramu 9,689.833 za dawa za kulevya, pikipiki 11, magari matatu na watuhumiwa 66 wakihusishwa na uhalifu huo.
Taarifa hiyo, imetolewa leo Januari 8, 2026 jijini Dar es Salaam na Jenerali wa Mamlaka hiyo Aretes Lyimo.
Amesema katika operesheni iliyofanyika Desemba mwaka jana jijini Dar es Salaam ambapo kwenye eneo la Sinza C mita wa Bustani nyumba namba 16, Jefferson Kilonzo Mwapande (35), raia wa Kenya, alikamatwa akiwa na gramu 131.88 za heroin.
Amefafanua kwamba mtuhumiwa huyo anadaiwa ameishi Tanzania tangu 2023, alitumia biashara ya kuuza chai kuficha biashara ya dawa za kulevya anayoifanya.
Aidha, katika mtaa wa Wailes, Temeke, jijini humo zilikamatwa pakiti 20 za skanka zenye uzito wa kilogramu 20.03 zikizimeta ndani ya bao la mbao na kufichwa kwenye bus aina ya Scania namba za usajili wa nchi ya Msumbiji namba AAM 297 CA.
"Bus hilo hutanya safari zake kati ya Nampula nchini Msumbiji na Tanzani, watuhumiwa waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo ni Amasha Iddi Mirisho (40), mkazi wa Buza, Dar es Salaam na Seleman Juma Ally (32), raia wa Msumbiji," amesema
Ameongeza kuwa katika eneo la Kinyerezi, Mtaa wa Mladoka wilaya ya Ilala, jijini humo watuhumiwa Erick Ernest Ndaga (32), Paul Blass Henry (34) na Tito Emanuel Mukude (35), walikamatwa wakiwa na bangi kg 193.66.
Pia amesema kutokana na ukaguzi uliofanyika kwenye kampuni za usafirishaji wa mizigo jijini Dar es Salaam, paketi 20 za dawa za kulevya aina ya mirungi zenye uzito wa kilogramu 9.54 zilikamatwa zikiwa zimetingwa kama majani ya mwaroani yaliyokaushwa zilizokua zikasafirishwa kutoka Kenya kuelekea Australia.
Pia ameongeza kuwa kupitia operesheni zilizofanyika katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Morogoro, Tanga, Lindi, Kilimanjaro, Njombe, Kigoma na Arusha zilikamatwa dawa za kulevya aina ya heroin gramu 37.34, skanka kilogramu 1.015, bangi kilogramu 7,969.98 na mirungi kilogramu 1,363.701 pamoja na kuketekezwa ekari 14 za mashamba ya bangi.
Ameweka wazi kuwa DCEA, inasisitiza wananchi kutoa taarifa kuhusu viashiria vya biashara ya dawa za kulevya na kuwa makini kutokubali kusafirisha mizigo isiyoijua. Mamlaka itaendelea na operesheni nchi nzima na kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wahalifu wa dawa za kulevya.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini, (LATRA), Halima lutavi amefafanua kuwa basi hilo ambalo limekamatwa lenye namba AAAM 297 CA haikuwa na reseni ya uendeshaji kwa hapa Tanzania ingawa awali walituma maombi na kupewa maelekezo kadhaa kwaajili ya kuliweka kwenye mfumo rasmi na hawakutimiza.
Hivyo ametoa wito kwa wamiliki wa magari ya usafiri kuacha kufanya vitendo kama hivyo kwani vinahujumu taifa na kuongeza kuwa LATRA itaendelea kushirikiana na mamlaka nyingine.





No comments:
Post a Comment