Kwa mujibu wa taarifa ya Bunge, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Azan Zungu (Mb) ametangaza kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Halima Idd Nassor kilichotokea Leo Jumapili Januari 18 Januari, 2026 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
“Kuwa masikitiko makubwa, natangaza kifo cha Mbunge wa Viti Maalum Halima Idd Nassor kilichotokea leo 18 Januari, 2026 Jijini Dar es Salaam. Natoa pole kwa Waheshimiwa Wabunge wote, familia ya Marehemu, ndugu jamaa na marafiki, Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Spika.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya Marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitatolewa hapo baadaye.





No comments:
Post a Comment