WAZEE WAJADILI AMANI, HAKI, KATIBA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, January 22, 2026

WAZEE WAJADILI AMANI, HAKI, KATIBA


NA MWANDISHI WETU

WAZEE kutoka taasisi mbalimbali nchini wanakutana leo jijini Dar es Salaam kujadiliana kuhusu maafa na uharibifu wakati wa uchaguzi, Katiba mpya uzalendo, haki, uwajibikaji na ujenzi, amani, utatuzi wa migogoro na maridhiano.


Mkutano huo wa majadiliano ulikuwa na washiriki zaidi 50 na umeandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), umejikita katika kuwapa nafasi wazee kujadiliana kwa njia ya busara kuhusu taifa lao.


Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa MNF, Joseph Butiku amesema wameamua kuainisha maeneo hayo manne kwa kuwa ndio kilio cha wananchi.


"Tumeamua kukutana sisi kama wazee kutoka makundi mbalimbali, ili tujadiliane kuhusu maafa na uharibifu wakati wa uchaguzi, Katiba mpya uzalendo, haki, uwajibikaji na ujenzi, amani, utatuzi wa migogoro na maridhiano," amesema.


Mzee Joseph Butiku amesema wazee wana uwezo wa kutambua changamoto za taifa, kuvumilia na kujadili mambo ya nchi, hivyo ni imani yake kikao hicho kitaweza kutoka na maazimio mazuri kwa maslahi ya nchi," amesema.


Butiku alisisitiza kuwa penye wazee haliharibiki jambo na kwamba fursa ya kukaa pamoja ni nguzo muhimu kwa maslahi ya nchi.


Mwenyekiti huyo amesema taifa lilipata tatizo kidogo baada ya miaka 65 hivyo wazee wanawajibu wa kukaa pamoja na kujadiliana namna ya kutoka hapo.


Amesema kwa miaka yote hiyo taifa limekuwa na umoja, upendo, amani na mshikamano, hivyo kilichotokea ni vema wakae wajadili na kuona namna ya kutoka.


Mwenyekiti huyo amesema Hayati Baba wa Taifa Nyerere alisema kazi iliyokuwa muhimu kwake tangu mwaka 1962 ni kujenga taifa lenye umoja kwa msingi wa heshima na usawa wa binadamu.


Mzee Butiku alinukuu maneno ya Rais Samia Suluhu Hassan alipozungumza na bodi ya MNF kwa kuwataka wafanye mambo mapya na kurejea katika nchi iliyokuwa inajengwa wakati wa mwanzo.


Rais Samia alisema anataka nchi yenye umoja, amani na mshikamano na kwamba MNF imeamua kubeba dhamana hiyo.






No comments:

Post a Comment