WASHUKIWA WATATU WA UJAMBAZI WAUAWA KWA RISASI SIMIYU - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, February 8, 2026

WASHUKIWA WATATU WA UJAMBAZI WAUAWA KWA RISASI SIMIYU



NA MWANDISHI WETU

JESHI la Polisi Mkoa wa Simiyu limefanikiwa kuwaua watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi baada ya kutokea majibizano ya risasi usiku wa kuamkia leo Februari 8, 2026, katika Wilaya ya Bariadi. 


Tukio hilo lilitokea baada ya polisi kupata taarifa kuwa wahalifu hao walikuwa wanavunja milango ya jengo la Simiyu Money Services kwa lengo la kuiba fedha za miamala ya kibenki na simu. 


Wahalifu hao walipoteza maisha wakiwa njiani kuelekea hospitali baada ya kujeruhiwa vibaya na risasi wakati wakijaribu kupambana na kikosi maalum cha polisi.


Katika eneo la tukio, polisi walifanikiwa kukamata silaha moja aina ya AK 47 ikiwa na risasi nane. Upekuzi uliofanywa ulibaini wahalifu hao walikuwa na fedha za kigeni zikiwemo shilingi mia tatu za Kenya na noti ya Misri, pamoja na tiketi za basi zinazoonyesha walitokea Migori nchini Kenya kuelekea Sirari na hatimaye Lamadi. 


Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limewashukuru wananchi kwa ushirikiano wao wa kutoa taarifa zilizosaidia kuzuia uhalifu huo mkubwa. 


Aidha, polisi wametoa onyo kali kwa watu wanaojihusisha na matendo ya kijinai, wakisisitiza kuwa operesheni na misako itaendelea ili kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unalindwa kwa gharama yoyote.

‎Credit ITV

No comments:

Post a Comment